Kesi za kijinai/madai dhidi ya wanawake ziangaliwe kwa jicho la 3, la sivyo tutahukumu wasio na hatia

Kesi za kijinai/madai dhidi ya wanawake ziangaliwe kwa jicho la 3, la sivyo tutahukumu wasio na hatia

Mhafidhina07

JF-Expert Member
Joined
Aug 1, 2014
Posts
3,340
Reaction score
4,659
Gender balance

Ni mtizamo au mfumo wa kuweka usawa wa kijinsia..kwa sasa dunia ipo katika kuchukua affirmative action kuitetea jinsia kwa kuamini kuleta usawa wa kijinsia lakini inaonekana ni silaha kubwa dhidi ya watu wenye ushawishi wa kifedha,kisera/siasa au kijamii ikiwa wataenda kinyume na matakwa ya kimfumo au njia moja wapo ya upigaji.

Kuna muda huwenda tukawa sahihi kuudidimiza mfumo dume ili kuleta usawa tunaodhania kuwa ni muhimu kwa dunia ya leo,lakini kuna misingi ya makosa tunayohukumu ina ukweli kiasi gani?

Kuna baadhi ya kesi hutengenezwa ili kushambulia na kuathiri maisha ya mtu binafsi ila inafikia kuathiri mfumo mzima wa maisha ya waliokuwa nyuma yake,sikatai kosa jawabu lake ni hukumu ila ni nani ambaye aliyefanyiwa hilo kosa?background ya hawa watu ipo vipi na nafasi ya mlalamikiwa ipo vipi katika jamii??tabia na mwenendo za aliyetendewa ziko vipi?.

Wasanii wakubwa wameshabambikiziwa kesi ila tunarudi pale pale mifumo ya kidunia ina ustawi hafifu wa jinsia ya kiume mizani mnayotumia kuwapima hao watoto wa 2000 mkumbuke kuwapima wanaume wa 70.

Nahitimisha
 
Back
Top Bottom