Salary Slip
Platinum Member
- Apr 3, 2012
- 49,390
- 152,301
Naamini ipo siku atatokea mtu jasiri ataeamua kutojitetea mahakamani pindi atapobaini mashitaka dhidi yake ni ya kubambikiziwa kwasababu tu ya chuki za kisiasa au vinginevyo.
Huweki Wakili unawaacha waendeshe kesi bila wewe kusema lolote halafu mwisho wa siku watoe hukumu waliokuwa wamepanga roho zao zisuuzike.
Narudiia, mtu wa kuandika historia ya aina hiyo yupo na siku moja atapatikana.
Kama tunavyosikia, mtu anatuhumiwa kutamka maneno haya au yanayofanana na haya: "safari hii tutakupa kesi ambayo hutachomoka" na mtu huyo wala hajitokezi kukanusha au hata kujitetea?
Mtu wa aina hiyo, siku akipatikana, huenda akawa chachu ya kubadili kabisa mifumo ya utoaji wa haki nchi hii na ataenda jela akiwa ameandika historia kubwa na ya kipekee kwa nchi hii.
Ipo siku.