Kevin Durant anabadili tu mademu

Ngoja afilisike ndio tutona uwezo wake wa kuwa sukari ya warembo.
 
wacha awale
jamaa yetu hasheem alicheza na hawa jamaa miaka ile 2013 wakati yupo okc
sjui yupo wapi sasa wenzake kd russels harden ibaka bado wanang'ara

Sent using Jamii Forums mobile app
 
KD ni hadimu kumuona akicheka au kutabasam, naona maduu wanazimika na ukauzu wake.
 
, CALIFORNIA, Marekani: NYOTA wa NBA, Kevin Durant, amezidi kwa warembo, kwani taarifa zinasema sasa anatoka na modo Sabrina Brazil.

Taarifa zinanyetisha kuwa mkali huyu wa timu ya Golden State Warriors amekuwa akitoka na mrembo Sabrina tangu alipotengana na mrembo mwingine, Cassandra Anderson.



KD, 30, pia amekuwa akihusishwa kimapenzi na mpenzi wa zamani wa Chris Brown, Amy Shehab pamoja na mwimbaji Keri Hilson. Durant alisitisha uhusiano wake na Cassandra, Oktoba, mwaka jana.

Lakini fowadi huyo pia aliachana na mchumba wake Monica Wright mwaka 2014 kwa madai ya kushangaza.



Alisema: “Nilikuwa na mchumba, lakini sikujua jinsi ya kumpenda, unajua ninachokisema? Tulitengana kwa staili hiyo.”

Lakini Monica, ambaye anacheza kikapu kwenye Ligi ya Wanawake Marekani (WNBA), alitoa sababu tofauti akidai walitengana kwa sababu ya imani yake kali kwa Mungu.



Mrembo huyo alisema: “Nilikosolewa sana kutokana na hilo, lakini nadhani Mungu alikuwa upande wangu. Kwa sababu nilishikilia kile ambacho najua ni kweli, hicho ndicho Mungu atanituza badala ya kile ambacho watu duniani w a naamini ni kizuri.”
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…