Ushangiliaji wa waTanzania kwa Ivory Coast jana ni uthibitisho kamili kuwa waTanzania hawajali ushindi wa nchi bali mtu/watu. Wanaona kushangilia Drogba ni bora zaidi (kwa kuwa ni mchezani wa Chelsea) kuliko kuishangilia timu ya Taifa.
Nadhani JK alikwenda kuangalia hilo. Nina imani atakuwa ameogopa sana kuona hali hiyo. Maana kama wananchi wakiendelea hivyo, basi ina maana watachagua mtu kwenye uchaguzi ujao badala ya chama, na kwa popularity yake, atakuwa matatani (kura zitapungua sana). Ila sijui nani atakaekuwa mpinzani wake. Maana anaitajika Drogba kumng'oa.
Wakuu tulipofungwa uwanja wote ulikuwa kimya. Tulipocheza vizuri tulishangalia. Drogba alizomewa. Mara he Drogba na wenzake wakaanza kushangiliwa. Mwishoni kabisa ndio kidogo tukawashangilia vijana wetu. Yaani tulikuwa hatueleweki kabisa!
Watanzania amuwajui si ni majuzi tu hapa nakumbuka Edibile Lunyamila akienda kwao Shinyanga mzee Lunyamila alikua anamfungia ndani kumuona T.Sh 50 na watu wanapanga mstari mrefu.
Hata huku tulipo dada ukimwambia nakupeleka Nando's duu ujue hiyo ni moja ya zile safari chache ambazo utamkuta tayari keshajitayarisha ukipiga horne tu mbio nje.
hahaha JC ya kweli haya
Ndio! Mechi ya jana kati ya Taifa Stars na Ivory Coast imedhihirisha hilo!Hakika 70% ya Watanzania ni 'Bendera Fuata Upepo! Habari ndio Hiyo!
.
Compa, Watanzania ni malimbukeni, hili ndio unalijua leo?. Baada ya uchaguzi mdogo Busanda na Biharamulo, nililisema, na nilishutumiwa kutukana watu bure!. Jana uwanja ulifurika, na kila tukipigwa chenga, uwanja unashangilia, tulipopigwa bao ndio kabisaaa. Hawa ndio sisi Watanzania na nchi yetu!.
Ndio! Mechi ya jana kati ya Taifa Stars na Ivory Coast imedhihirisha hilo!Hakika 70% ya Watanzania ni 'Bendera Fuata Upepo! Habari ndio Hiyo!
Kuyumbayumba kule ni kielelezo cha ukosefu wa msimamo/mwelekeo wa wananchi na nchi!
Kwani kabla ya mechi ni nani aliyekuambia anaenda kuishangilia timu moja tu? Maybe waliofanya hivyo huo ndio msimamo wao, na huwezi ukasema hawakuwa na msimamo wakati msimamo wao ulionekana dhahiri. Au unadefine vipi msimamo?Ungekuwa uwanjani ungeelewa mkuu, kwa asilimia kubwa Watanzania hawana msimamo!
Kwani kabla ya mechi ni nani aliyekuambia anaenda kuishangilia timu moja tu? Maybe waliofanya hivyo huo ndio msimamo wao, na huwezi ukasema hawakuwa na msimamo wakati msimamo wao ulionekana dhahiri. Au unadefine vipi msimamo?