Bilionea Asigwa
JF-Expert Member
- Sep 21, 2011
- 16,515
- 28,506
Malkia wa nyimbo za mwambao Afrika Mashariki na kati, Khadija Omary Kopa amesema sio jambo zuri kwa wanawake kukaa kugombea mwanaume na kuwataka wawe wabunifu katika mapishi pamoja na kutumia nyonga zao ili mwanaume mwenyewe apagawe nasio kukaa kugombana.
Khadija Kopa ametoa kauli hiyo wakati alipokuwa anazungumza kwenye kipindi cha kikaangoni kinachoendeshwa na EATV.
“Unapiganaje na mke mwenzio?, yeye akirusha risasi wewe rusha atomic. Yeye akimpigia bwana chapati wewe piga mkate wa ufuta, kuku na ndizi za kupaka. Sasa unagombanaje na mke wenzako ?,hakuna haja ya kugombana na mke mwenzio wewe fanya vitu ili mwanaume azidi mapenzi upande wako. Watu wa siku hizi hawajui bajeti ya mapenzi kazi kufofoka tu”, amesema Khadija Kopa.
Pamoja na hayo, Khadija Kopa ameendelea kwa kusema “tengeneza mambo yako nyumba inukie mambo yawe motomoto na uchangamfu kama kawaida akija mume wako afurahie, hakuna haja ya kugombana gombana kila siku wewe zidisha mavitu ili mwanaume achenguke, fahari ya mwanamke nyonga vitu vingine majaliwa”.