Mbunge wa viti maalumu katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Khadija Taya maarufu kwa jina la Keisha amesema kwa muda wa miaka 14 vyama vya watu wenye ulemavu havikuwahi kupewa fedha za ruzuku za kujiendesha, na kwamba kuanzia mwaka 2023/2024 ilipatikana bajeti ya shilingi bilioni moja kwa ajili ya vyama hivyo.
Keisha ameyasema hayo katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC), wakati wa kongamano la kumpongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutimiza miaka minne ya kuliongoza Taifa la Tanzania.
Amesema Rais Samia Suluhu Hassan pia ametoa fedha kwa ajili ya manunuzi ya mafuta maalumu ya kujipaka kwa watu wenye Ualbino ambayo yanapatikana kwenye halmashauri zote nchini kwa sasa.