N'yadikwa
JF-Expert Member
- Aug 10, 2014
- 7,427
- 10,905
Kwa wafuatiliaji vyombo vya habari na wasikilizaji wa habari lakini pia wanaofuatilia kuwafahamu watangazaji jina la Khalid Gangana sio geni masikioni mwao na machoni mwao.
HISTORIA YA KHALID GANGANA KWA UFUPI
Kijana huyu alianza kazi ya utangazaji akichipukia yaani a humble beginning akiwa na kituo cha Mlimani Television mwaka 2010 - 2011 kijana huyo hapo Mlimani TV alikuwa akifanya kipindi cha Ladha Bomba cha wanamuziki hasa wa kizazi kipya. Ni katika kipindi hiki ndipo nilibaini kwamba kijana huyu atafika mbali katika tasnia ya utangazaji na uandishi wa habari.
Baada ya kutoka Mlimani TV kijana huyu msomi wa Shahada ya Uandishi wa Habari kutoka Chuo Kikuu cha Dar es salaam alifanya kazi na vituo kadhaa binafsi kikiwemo kituo cha Sasemi ambayo kimsingi ni kampuni ya utayarishaji maudhui chini ya jamaa mmoja wa huko SJMC.
Hatimae kijana huyu akaibukia TBC 1 ambako anafanya vizuri hadi sasa.
Kwa masikio yangu nilimsikia wakati mmoja akibainisha kuwa alikuwa na ndoto ya kuwa mtangazaji wa kimataifa, huku roli modo wake/mtu wa fani anaemvutia akiwa ni Salim Kikeke (hata yeye huyu kijana ukimtazama ana swaga za Kikeke fulani hivi).
Moja mambo imara kwa kijana huyu katika tasnia ni umahiri wake wa kuuliza maswali na kupangilia muonekano wake katika television.
Bwana mdogo nakutakia kila la kheri. Fahamu unawa inspire vijana wenzako wengine kuwa mfano bora wa utangazaji na uandishi habari wenye umahiri. Wewe pamoja na Millard Ayo ni miongoni mwa vijana ninaowastahi kwa kuenzi misingi ya Uandishi wa Habari wenye kuzingatia maadili hapa Tanzania.
Mungu akubariki Khalid Gangana.