Mkalukungone mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 862
- 1,755
Bado huyu jamaa ambaye anasota na kesi ya mauwaji ya mke wake. Lakini kila wakati ananiacha mdowo wazi na maswali mengi kwa namna anavyojibu na kuikwepa kesi yake hii.
Leo kasema mengine Alidai kuwa mawakili wa serikali wanataka ahukumiwe kunyongwa, akihoji "vipi nikihukumiwa kunyongwa halafu baadaye mke wangu akatokea?
MFANYABIASHARA Khamis Luwongo (38) amedai mahakamani kuwa alilidanganya Jeshi la Polisi kwamba alimuua na kuchoma moto mwili wa mke wake Naomi Marijani kutokana na mateso aliyokuwa akiyapata, hivyo ameomba aachwe huru akamtafute kwa kuwa yupo hai.
Pia amedai kuwa upande wa Jamhuri pamoja na Mkemia Mkuu wa Serikali wameshindwa kuthibitisha kwamba aliyefariki dunia ni Naomi kwa sababu hakuna majibu ya vinasaba (DNA) yaliyoonesha hivyo katika ripoti iliyoletwa na shahidi.
Luwongo alidai hayo hayo juzi mbele ya Jaji Hamidu Mwanga wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam huku akiongozwa na Wakili wake, Hilda Mushi wakati anatoa utetezi wake katika kesi ya mauji ya mke wake inayomkabili.
Soma Pia:

- Anayeshtakiwa kumuua Mkewe asema Kichwa cha Mwanamke huyo kiliungua moto kirahisi sababu alikuwa anakigeuza
- Mahakamani: Aliyemchoma mkewe kwa magunia mawili ya mkaa anatajwa kuwa mlemavu wa akili