Khloé Kardashian: Kila mtu alikuwa uchi Kwenye Party za P Diddy

Khloé Kardashian: Kila mtu alikuwa uchi Kwenye Party za P Diddy

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
2,060
Reaction score
5,648
Khloé Kardashian amezungumzia sherehe za Sean “Diddy” Combs kwenye kipande cha episode ya “Keeping Up With the Kardashians” kilichoibuliwa baada ya msanii huyo kukamatwa kwa tuhuma za usafirishaji wa watu kwa ajili ya kuwatumikisha kingono.

Mwanamitindo huyo, mwenye umri wa miaka 40, alikumbushia kuhudhuria moja ya sherehe za kifahari za Diddy kwenye kipindi hicho kilichorushwa Agosti 17, 2014. Khloé aliwaambia dada yake Kourtney Kardashian na rafiki yao Khadijah Haqq kuwa sherehe hiyo ilikuwa na watu wengi waliokuwa hawajavaa nguo.

1727185318465.png

Sherehe za Diddy zilikuwa maarufu kwa kuvutia mastaa wengi kama vile Justin Bieber, French Montana, na Quincy Combs. Khloé alielezea kuwa hakuweza kulala baada ya kuhudhuria sherehe hiyo iliyofanyika hadi alfajiri, akiongeza kuwa Kourtney angefurahia kuona watu wakivua nguo.

Wiki iliyopita, Diddy, mwenye umri wa miaka 54, alikamatwa New York na kufunguliwa mashtaka ya kula njama, usafirishaji wa watu kwa njia ya udanganyifu, na usafirishaji kwa ajili ya ukahaba. Mashtaka hayo yanadai kuwa msanii huyo aliendesha biashara haramu kwa muda mrefu ili kutimiza matakwa yake ya kingono na kuficha matendo yake.

Pia, Soma: Diddy anyimwa dhamana na Mahakama, alitoa ofa ya bilioni 135
: Diddy aripotiwa kuwekwa katika uangalizi maalum kuepusha asijiue

Wakili wa Diddy alisema kuwa mashtaka hayo si ya haki na wanamvunja moyo kutokana na hatua ya ofisi ya mwendesha mashtaka kuendelea na kesi hiyo. Hii si mara ya kwanza Diddy kukumbwa na tuhuma kama hizo, kwani mwaka 2023, mpenzi wake wa zamani, Cassie Ventura, alimshtaki kwa madai ya ubakaji na unyanyasaji wa kimwili, ingawa walifikia makubaliano.

1727185257995.png

Diddy sasa anakabiliwa na mashtaka mengine kutoka kwa wanawake wengi, ikiwa ni pamoja na Dawn Richard, aliyedai kuwa alishuhudia unyanyasaji wa kimwili dhidi ya Cassie wakati walipokuwa wakifanya kazi pamoja.
 
Wakubwa salam zenu.

Hakika duniani kuna watu na matukio-mzee Sean Combs aka Puff Daddy yupo matatani sasahivi.

But kikubwa hebu tuziangazie zile party zake alizokuwa akiziandaa kwa gharama kubwa zijulikanazo kama "Freak Off" na yaliyokuwa yakiendelea background.

Inasemekana watu mbalimbali wakiwemo, matajiri wakubwa, wanasiasa wakubwa, mafootbaler, ma-actor na ma actress wazee wa vikapu na wengine kibao wameshawahi zama kwenye party za mzee didi na wapo on record

Inasemekana ukizama kwenye Pati zake ukinywa vinywaji viwili vitatu akili inawaka. Unaweza ukafanya mambo ambayo hata hukutarajia.

Ni kawaida sana kukuta wanawake wengi warembo wakiwa uchi kwenye hizo Pati watu walikuwa wanafanya uchafu wa kila aina unao relate na mwili wa binadamu. Kumbe muhuni jumba lake lote lina hidden cameras

Inasemekana hata Steve Harvey wale wanaomfahamu alishafanya jambo la kijinga kule akawa recorded kwenye moja ya vyumba akapigwa blackmail ya ajabu. Baadae binti yake Lory Harvey akaja kuwa chakula cha mtoto wa Sean Combs na Sean Combs mwenyewe akapita nae vile vile

Haya sio mambo mazuri kabisa

Tuache mambo mabaya kwa ustawi wa jamii zetu
 
Unaleta tabia za kupenda kitonga unaalikwa alikwa kwenye sherehe ambayo hujui gharama zake alafu unaenda kama nyumbu lazima uzilipie indirect
 
Ikitokea mwamba mmoja mwenye uthubutu akaanzisha hiyo party huku kwetu, tutashuhudia mengi sana yakivuja.

Maana bila hata ya kuwa na hizo freak off parties, wasanii na watu maarufu wa Kibongo wanafanya uchafu mno nyuma ya mapazia. Sasa imagine pakitokea sehemu rasmi ya kuwa na hiyo party halafu kutegwa camera.
 
Zipo Sana tu ila ndo haujajua kama zipo!
 
Ikitokea mwamba mmoja mwenye uthubutu akaanzisha hiyo party huku kwetu, tutashuhudia mengi sana yakivuja.

Maana bila hata ya kuwa na hizo freak off parties, wasanii na watu maarufu wa Kibongo wanafanya uchafu mno nyuma ya mapazia. Sasa imagine pakitokea sehemu rasmi ya kuwa na hiyo party halafu kutegwa camera.
Hivi binti kidimbwi hayafanyiki hauo ?
 
Back
Top Bottom