Kiafya Binadamu anatakiwa kutumia muda gani kwa kutoa haja kubwa chooni?

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2013
Posts
60,660
Reaction score
121,325
Madaktari mliopo humu Jamvini tunaomba msaada wenu tafadhali kwamba Kitabibu au Kiafya Binadamu anatakiwa kutumia muda gani Kutoa Haja Kubwa yake pindi awapo Chooni kwani kuna mahala fulani nimeona Watafiti fulani hivi wakisema kwamba muda unaotakiwa Mtu Kuutumia huko ni dakika 3 tu na ukichelewa sana basi ziwe 5 na kama ukizidisha hapo basi utakuwa na matatizo ya Kiafya.

Nimelileta hili Kwenu ili nyie Madaktari mtusaidie kutupa ufafanuzi wa Kitaalam kwani hapa ' Kitaani ' nilipopanga kuna ' Mabrazameni ' wawili hivi wao wakiingia tu Chooni kutoa hiyo huduma ya Haja Kubwa unaweza ukaangalia Taarifa ya Habari nzima ya ITV na ukaongezea na ile ya BBC inayorushwa na Star tv kwa Nusu saa na bado akawa hajamaliza.

Je Madaktari kuna ukweli wowote hapa?

Nawasilisha.
 
hao watakua wanatumia mirungi.wanaotumia mirungi chooni wanakaa muda sana hahaha sijui gogo wanapolikata huwa halitoki kwa muda muafaka
 
Nitarudi baadaye nione wataaramu wamesemaje ili nami nijipime
 
Umefikiria nje ya box, sijawahi ku-relate time ya kutoa haja kubwa na afya, nilidhani time inayotumika inakua na uhusiano na quantity na quality ya mzigo ulioubeba tumboni. kama zege yako ni rojo rojo basi nilidhani utatumia muda mfupi kidogo na kama iko kavu unaweza ukatumia muda mrefu zaidi. Kikubwa ni namna gani unaweza ukaifanya zege yako kuwa responsive to effective utilization of time. Ngoja tupate madini kutoka kwa wajuzi zaidi.
 
Umeuliza swali zuri na ambalo limeamsha hoja nzuri pia.lkn ni kama ulivyosema dk 3 hadi 5 mtu unaweza ukawa umemaliza haja zako ktk hali ya kawaida.lkn wengine huchelewa sana kutokana na matatizo mbali mbali moja wapo ikiwa ni kupata haja kubwa iliyongumu (constipation) ambayo huchangiwa kwa kiasi kikubwa na ulaji wetu tunakula kwa mazoea na si kiafya.lkn pia kuharisha nako mtu unaweza kaa muda mrefu kutokana kujaribu kutaka kutoa haja yote na unapotaka kutoka unahisi bado hujamaliza lkn hii ni kula chakula kichafu ni tofauti na ulaji ule wa kusababisha ukapata choo kigumu.

Aya nami niwaulize kama mtu unapata haja kubwa ya kawaida na bila kutumia nguvu wala kutoka jasho je kwa siku angalau uende chooni mara ngapi??
Hahah maana mwingine yy kila baada ya siku mbili au tatu ndiyo apate choo na ulaji wake n wa kawaida tuu sasa je anatatizo huyu nae au lah??
 
Mimi si daktari lakini kutoa haja kubwa kunatwgemea.
1. Unywaji wa maji,
2. Vyakula unavyokula
3. Matunda
4. Activities za mwili wako
5. Kama una tumia dawa hasa za kupunguza maumivu

Haja kubwa hutengenezwa kwa 75% ni maji na 25% ni solid matter. Ukifika kwenye colon haja kubwa inapata shape na kama hunywi maji ya kutosha matatizo ya constipation hujitokeza. Jijengee tabia ya kunywa litre mbili za maji kila siku utausaidia szna mwili wako kwenye digestion, transportation na kutoa waste products.

Vyakula yenye fibre husaidia sana kupata haja kubwa murua. Ugali wa dona, makande, maharage, mkate wa brown pamoja na wali wa brown, mchicha, cabbage, nk. Vyakula hivi pia husafisha utumbo mpana (colon)

Matunda kama machungwa, mananasi, apples, pears nk pia vina fibre.

Kufanya mazoezi pia husaidia mambo kuendelea mwilini. Uneshaona wazee na wagonjwa wanalalamika kutokupata choo kwani muda mwingine wanakuwa wamekaa au kulala. Ukiwa mtu wa jogging mzigo hautakupa shida kuushusha.

Kama unazingatia yote haya ni kweli dakika tatu tu unakuwa umemaliza shughuli
 
Haja kubwa ndo Mavi?
 
Kukaa siku mbili bila kupata choo na unakula chakula sio sahihi kwa binadamu alie hai na mwenye afya ukimaliza kula chakulatu mmeng'enyo unaanza kufanyika na mmeng'enyo ukikamilika unatakiwa upate choo ikiwa kinyime na hivyo basi unatatizo la kiafya
 
Hata mimi sio Dr ila najua kuna Makundi makuu 7 ya Haja kubwa(mavi) Rejea Bristol Stool Chart.
Mimi huwa napata type 4 ambayo ki afya ni nzuri..sijui huwa natumia dk ngapi, ila kwangu ni rahisi tu labda hata dk mbili.
 
Hata mimi sio Dr ila najua kuna Makundi makuu 7 ya Haja kubwa(mavi) Rejea Bristol Stool Chart.
Mimi huwa napata type 4 ambayo ki afya ni nzuri..sijui huwa natumia dk ngapi, ila kwangu ni rahisi tu labda hata dk mbili.
Turejee wapi hiyo bristol tool chart?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…