1. Kupenga kamasi kunahitaji umakini vinginevyo waweza kujiletea madhara kwenye mfumo wako wa pua, masikio na hata koo ( ENT).Kumbuka makamasi au Mucous iliyoko puani huchuja vijidudu vilivyomo hewani vyenye kuleta uambukizo. Wataalamu wa tiba wa ENT hushauri kuwa pressure inayotokea unapopenga huweza kuathiri mishipa damu na huathiri mfumo wako wa hewa, hivyo tunatakiwa kuwa makini tunapopenga.
2. Ili kupunguza madhara, kama alivyosema Gaijin hapo juu, unatakiwa kupenga ukiwa umeziba pua moja ( one nose at a time)..ili kusiwe na pressure kubwa sana puani, maskioni na hata kichwani... nadhani mtakubaliana nami kuwa unapokuwa na mafua ukapenga wakati mwingine unajisikia kama ubongo nao unataka kutoka lol!.
3. Penga kwa kutumia kitambaa safi ( epuka kurudiarudia kitambaa maana utajiletea uambukizo), au penga kwa kutumia tissue. Ukiwa unaoga au kunawa uso usiogope kupenga kwa mkono. Infact njia nzuri zaidi ya kupenga ni kwa kutumia maji ya uvuguvugu yenye chumvi ukavuta mvuke na kusaidia kutoa mafua. Hapo kwa vyovyote utatumia mikono yako na inabidi unawe vizuri baada ya hapo. Njia ya kupenga kwa mikono hata hivyo siyo sahihi uwapo nje ya nyumbani kwako au sehemu utakayopata maji na sabuni ya kunawa.