Mzizi wa Mbuyu
JF-Expert Member
- May 15, 2009
- 7,375
- 6,958
Unayavutavuta kwa ndani then unayatelekeza kwenye aliemntary canal...!!!!
Kwani utotoni mama alikufundisha ufanyeje wajemeni?
Kibongo bongo watakuambia kinyaa lakini ndio ukweli na utaratibu wa kupenga makamasi kiafya na kistaarabu ili husimwambukize mwingine. Mada nzuri sana hiiupengaji wa mafua kitaalamu unatakiwa upenge kwa kuziba tundu moja na usitumie nguvu kuyatoa.
pili unatakiwa mafua ukiwa nayo uyatowe, kwa sababu usipoyatoa yaani yale ma germs yote unayarudisha ndani ya mwili wako
suala gumu linaguja upengee wapi? wenzetu ulaya hutembea na paketi vya tissue, unapenga kama hakuna dust bin unatia katika mfuko wa plastik unaufunga unatia kweenye handbag yako unatembea nayo mpaka ufike nyumbani
holla!
Asante Mama WOS1. Kupenga kamasi kunahitaji umakini vinginevyo waweza kujiletea madhara kwenye mfumo wako wa pua, masikio na hata koo ( ENT).Kumbuka makamasi au Mucous iliyoko puani huchuja vijidudu vilivyomo hewani vyenye kuleta uambukizo. Wataalamu wa tiba wa ENT hushauri kuwa pressure inayotokea unapopenga huweza kuathiri mishipa damu na huathiri mfumo wako wa hewa, hivyo tunatakiwa kuwa makini tunapopenga.
2. Ili kupunguza madhara, kama alivyosema Gaijin hapo juu, unatakiwa kupenga ukiwa umeziba pua moja ( one nose at a time)..ili kusiwe na pressure kubwa sana puani, maskioni na hata kichwani... nadhani mtakubaliana nami kuwa unapokuwa na mafua ukapenga wakati mwingine unajisikia kama ubongo nao unataka kutoka lol!.
3. Penga kwa kutumia kitambaa safi ( epuka kurudiarudia kitambaa maana utajiletea uambukizo), au penga kwa kutumia tissue. Ukiwa unaoga au kunawa uso usiogope kupenga kwa mkono. Infact njia nzuri zaidi ya kupenga ni kwa kutumia maji ya uvuguvugu yenye chumvi ukavuta mvuke na kusaidia kutoa mafua. Hapo kwa vyovyote utatumia mikono yako na inabidi unawe vizuri baada ya hapo. Njia ya kupenga kwa mikono hata hivyo siyo sahihi uwapo nje ya nyumbani kwako au sehemu utakayopata maji na sabuni ya kunawa.
Angalizo kwenye tissue. Sio tissue za aina zote zinafaa kutumika kupengea makamasiTissue is the best (coz hakuna haja ya kufua). Kuna aina za tissue ambazo zina vumbi kidogo sana (maana hata kitambaa kina vumbi to some extent). Kitambaa, licha ya kutembea na mafua yako kutwa nzima mfukoni, pia nadhani inasababisha multiple infections(lolz!). Ila kupenga/kufyatua waziwazi ni kusababisha maambukizi kwa wengine na ni uchafu uliokithiri. (Bora umeze hehehe!🙄)
Angalizo kwenye tissue. Sio tissue za aina zote zinafaa kutumika kupengea makamasi
Kamanda MM, hii si ndiyo yenyewe Kibongo bongo. Kwa mfano niko Kariakoo sokoni, kama vile nina mafua na kuna jua la kufa mtu na uchumi wenyewe ndio huo unagonga pande zote mfukoni nina Anjifu moja tu, nitafanyaje halafu katika zunguka zunguka nimekutana na Ngosha mwenzangu, kweli nisimpe mkono Mkuu. Je nikikutana na Mama Mkwe je, nimpotezee vilevile.Watu wabaya ni wale wanaopenda kwenye hendikachifu halafu wanaitumia kutwa nzima huku wakiigeuza upande upande na jasho likiwatoka wanajipangusia usoni! halafu anakuja na kukusalimia!!!
hii ushauri imetulia sana, acha tuiweke kwenye makabrasha itusaidie msimu wa vumbi kali , senksi greti thinka.1. Kupenga kamasi kunahitaji umakini vinginevyo waweza kujiletea madhara kwenye mfumo wako wa pua, masikio na hata koo ( ENT).Kumbuka makamasi au Mucous iliyoko puani huchuja vijidudu vilivyomo hewani vyenye kuleta uambukizo. Wataalamu wa tiba wa ENT hushauri kuwa pressure inayotokea unapopenga huweza kuathiri mishipa damu na huathiri mfumo wako wa hewa, hivyo tunatakiwa kuwa makini tunapopenga.
2. Ili kupunguza madhara, kama alivyosema Gaijin hapo juu, unatakiwa kupenga ukiwa umeziba pua moja ( one nose at a time)..ili kusiwe na pressure kubwa sana puani, maskioni na hata kichwani... nadhani mtakubaliana nami kuwa unapokuwa na mafua ukapenga wakati mwingine unajisikia kama ubongo nao unataka kutoka lol!.
3. Penga kwa kutumia kitambaa safi ( epuka kurudiarudia kitambaa maana utajiletea uambukizo), au penga kwa kutumia tissue. Ukiwa unaoga au kunawa uso usiogope kupenga kwa mkono. Infact njia nzuri zaidi ya kupenga ni kwa kutumia maji ya uvuguvugu yenye chumvi ukavuta mvuke na kusaidia kutoa mafua. Hapo kwa vyovyote utatumia mikono yako na inabidi unawe vizuri baada ya hapo. Njia ya kupenga kwa mikono hata hivyo siyo sahihi uwapo nje ya nyumbani kwako au sehemu utakayopata maji na sabuni ya kunawa.
tukiongelea mambo ya tissue kuna yule wa kijijini hata haifahamu, yeye nae ni wa kumuangalia pia na kushauriwa apengeje maana nako kule...mmmh!!