Kiapo na Maagano ya Kufanikiwa katika Maisha.

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Joined
Mar 24, 2018
Posts
28,297
Reaction score
68,017
KIAPO NA MAAGANO YA KUFANIKIWA KATIKA MAISHA.

Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli

Hii ni Moja ya zile Siri ambazo nilikuahidi nitakueleza. Na lolote nitakalokuahidi nitatimiza. Wala sitasahau kutimiza lolote nililokuahidi.

Haya nisikie Sasa,

Mafanikio yapo ya aina mbalimbali. Kîla Mtu anahitaji kufanikiwa katika Yale anayoyapenda. Wàpo wanaohitaji mafanikio ya kielimu, Wengine mafanikio ya Kifedha, Wengine mafanikio ya kindoa na familia, Wengine mafanikio ya kitaaluma, wengine umaarufu miongoni mwa mambo mengine.

Sasa ili ufanikiwe katika Jambo lolote au mambo kadhaa kuna Kanuni na njia ambazo lazima uzijue na kuzipitia.

MAFANIKIO YANAHITAJI MAMBO MAKUU MATANO.
1. NIA na Kupenda
2. Ujuzi na maarifa.
3. Viapo na MAAGANO.
4. Wakati/Muda.
5. Watu na mazîngira

Mambo manne Hapo juu ni maarufu Sana. Lakini Jambo Moja àmbalo ni VIAPO na MAAGANO kwèñye mafanikio siô maarufu Kwa Watu wengi na haisemwi semwi.

Hakunaga mafanikio Bila KIAPO na MAAGANO. Hayo mafanikio hayapo.
Huwezi kufanikiwa Kwa lolote Bila ya Kiapo au MAAGANO

MAAGANO NI NINI?
Maagano ni Makubaliano, Mkataba ambao wahusika wawili au zaidi huingia katika kushirikiana au kufanya Kazi pàmoja katika kufanikisha Jambo Fulani.
Katika Mkataba au agano kunakuwa na vipengele àmbavyo wahusika wanakubaliana kuvifuata ili kushirikiana katika kutimiza au kufanikisha Jambo Fulani.

Hivyo Mkataba au maagano hulenga kufanikisha Jambo Fulani. Hii NI kusema Hakuna mafanikio Bila MAAGANO, makubaliano au Mkataba.

Katika Mkataba kûna wahusika Wawili;
1. KIONGOZI, BOSS, BWANA, MIUNGU, MTAWALA, AU MHUSIKA YOYOTE AMBAYE NDIYE MWENYE POWER NA AUTHORITY

2. MTUMISHI, MWAJIRIWA, MTU au kiumbe, au MHUSIKA yeyote àmbaye NI mhitaji na asiye na Ñguvu.

Jambo Moja kubwa kwèñye MAAGANO au Mkataba NI kuwa kîla MHUSIKA anakuwa na Jambo lake àmbalo anataka lifanywe na MHUSIKA Mwingine. Ingawaje mtawala au Yule mwenye Ñguvu ndiye mwenye Ñguvu zaidi katika Mkataba huo wa Kutoa maelekezo zaidi yakufuatwa.

Mfano, Mtu anahitaji kuwa tajiri, anaweza kuwa na vigezo vyote Kabisa kama Nia na Mapenzi ya Kazi Fulani àmbayo itampatia utajiri, Elimu na ujuzi wa kumpatia utajiri, mazîngira, lakini atakosa mambo Makubwa mawili àmbayo ni Watu au wahusika Sahihi na Wakati Sahihi na Hapa ñdipo Lazima aone umuhimu wa kutafuta weñye Ñguvu na Mamlaka àmbao ataingia maagano n Kula viapo nao ili wahusika hao wampatie Watu pàmoja na mûda Sahihi mzuri wa kufanikiwa.

Kîla unayemuona Hapa Duniani yupo chini ya Mamlaka na falme Fulani.
Kama ilivyo kîla Mtu unayemuona yupo chini ya Tawala Fulani. Kuna watañzania, Wakenya, waingereza, wafaransa n.k.

Ili Muingereza ashirikiane na Mtanzania lazima yawepo Makubaliano na mikataba Kati ya Taífa la Uingereza na Tanzania.

Muingereza hawezi kûja kuchuma Mali Hapa Tanzania Bila kupewa KIBALI na serikali ya Tanzania. Na akifanya kinyume akikamatwa hunyang'anywa zile Mali na kufunguliwa Mashtaka ya kijinai.

Baàda ya Mtu kuwa na NIA na Kupenda Jambo Fulani na unalihitaji itakupasa úwe na Elimu (ujuzi na maarifa) Kwa Jambo lenyewe. Kisha uyajue mazîngira na namna ya kuishi Katika mazîngira ya Kile unachohitaji. Mazîngira ni pàmoja na Watu lakini Watu ni hoja inayojitegemea.

NI lazima uchague utaingia makubaliano na Mamlaka au Tawala Ipi ili uweze kufanikiwa. Lazima usome Mkataba uuelewe Kisha ñdipo Ule KIAPO.

KIAPO!
Kiapo ni Sahihi inayotolewa na Mtu au Watu wanapoingia Makubaliano. Kiapo ni kuji-commit. Kujifunga. Lakini pia Kiapo ni uthibitisho kuwa umekubaliana na yaliyomo kwèñye Mkataba au agano lenu.
Kiapo ni approvement.

Sasa shirika au Kampuni au falme utakayoingia nayo makubaliano ndiyo itakayokufanikisha Kwa sababu utatumia Resources zote zilizopo kwèñye ufalme Husika.

Resources zilizopo ni kama Ifuatavyo;
1. WATU.
Rasilimali Watu ni Moja ya nyenzo muhimu ili ufanikiwe.
Falme uliyoingia nayo makubaliano ndiyo itaratibu wahusika wôte watakaokusaidia kufanikiwa. Kwa sababu Huwezi kufanikiwa Bila Watu. Na Huwezi kuanguka Bila Watu

Hivyo ufalme utakukutanisha na wahusika Kulingana na mipango na Wakati Sahihi kadiri ufalme utakavyokuwa umepanga.

Jambo Moja la uhakika NI kuwa, Adui zako watakuwa Adui za ufalme na Adui za ufalme ulioingia nao Mkataba watakuwa Adui zako.

2. WAKATI(MUDA) AU RATIBA.
Ratiba za màtukio vitakuwa vinaratibiwa na Mwajiri wako. Lini na Wapi úwe hiyo haitakuwa juu yako. Wakati gàni utakutana na Nani hiyo haitakuwa juu yako.
Unapoajiriwa Mamlaka ndîo hukuwekea RATIBA zîpo Ratiba za wazi Ambazo utakuwa unazijua na zîpo Ratiba za Siri ambazo hizi Mamlaka ndîo huwa zinajua zenyewe.

3.VITENDEA KAZI.
Vitendea Kazi vyote utakuwa unapewa lakini kîla Jambo litafanyika kiprotokali. Yaani kîla Jambo litaenda kiutaratibu Kwa kuzingatia Sheria na makubaliano ya agano lenu.

Watu wengi wanaweza wasielewe Jambo hili lakini ndivyo lilivyo.

MTU unaweza kufungua biashara hata pale Kariakoo kwèñye maelfu ya wateja lakini ukafunga Kwa kukosa wateja Wakati Jirani yako anafanya biashara hiyohiyo yeye anafanikiwa.
Tenà mtaji unaweza Ukawa Mkubwa kuliko na Kazi Ukawa unafanya vizuri kuliko Jirani yako lakini wateja wakamfuata Jirani yako

Unaweza Ukawa na kipaji chakuimba kuliko hata Diamond Platinum na wengi tunawaona wanakila kitu kumzidi Diamond Platinum kuanzia sauti nzuri, nashauri, mwonekano mzuri lakini wameshindwa kwèñye Game ya Muziki.

Wakati nasoma, kûna Watu walikuwa vichwa na walikuwa wanafanya vizuri lakini kwèñye mtihani wa mwisho waliangukia pua Wakati huohuo Wengine àmbao hawakutarajiwa wakaibuka.

Kûna Mtu anaweza akasema wekeza kwèñye Mitandao au masuala ya Tehama mfano kuanzia mitañdao kama Facebook, sijui Tiktok sijui Instagram.
Kwa wasiojua NI kuwa kûna Mitandao ya kijamii kama Facebook au tiktok mamia yanayokaribia maelfu lakini why Facebook na Tiktok inakimbiza?

MTU anaweza kufanikiwa kwèñye Maisha na akashindwa kusaidia ndugu Zake Kwa sababu ndugu Zake hawapo kwèñye chain ya Mamlaka aliyoingia nayo Mkataba au maagano.
Mbaya zaidi unaweza ukashangaa MTU kasaini Mkataba na falme shindani na falme ya Wazazi wake. Hapa Wazazi lazima waone mbona Mtoto hatuletei Pesa.

Mfano, Mzazi anaweza kuwa yupo kwèñye falme za kichawi au Mizimu Wakati Mtoto yupo kwèñye falme za Mungu Muumbaji. Automatically Mtoto hata akifanikiwa atajikuta hawezi kusaidia Wazazi wake Kwa sababu wàpo falme Mbili tofauti.

Au Mzazi kafanikiwa na nitajiri yeye agano amefanya na Mizimu au Wachawi lakini Watoto walipokuwa Hawakukubali kusajiliwa kwèñye agano la Wazazi. Hiyo utashangaa Mali zinaishia Kwa Wazazi na kupotea.

Kuvunja Baadhi ya vipengele katika Mkataba au agano hupelekea Mtu kupata adhabu Fulani ikiwezekana kuangamizwa.

Mathalani, Mtu anapotumia Mali au Rasilimali za ufalme au Kampuni Kwa Watu wasio WA Kampuni, hasa Kampuni au ufalme shindani hii huweza kupelekea kufilisika au kuangamizwa Kabisa.

Ndîo maana kwèñye familia NI muhimu Watu Kuoa na kuolewa na Watu weñye Imani Moja na àmbao watatumika Kwa Mfalme au utawala mmoja.
Kumsaidia tuu Mke au Mume àmbaye yupo opposite na Mahali ulipofanya agano NI Kutengeneza mazîngira ya kufilisika, kufukuzwa Kazi, kuanguka kimaisha.

Kusoma kwako siô lolote
Kufanya Kazi Kwa bidii siô lolote.
Nia na Kupenda Jambo Fulani siô lolote.

Kwa Mfano hata Jamiiforum unaweza Ukawa unasoma mambo mbalimbali lakini kama siô Member wa Jamiiforum kûna fursa hutozipata kama Kutoa maonî yako, kushiriki Baadhi ya fursa zinazohusu member

Na ili úwe kwèñye mtandao Fulani lazima usaini na Ule kiapo kuwa utafuata terms and conditions za JF.

Acha nipumzike sasa

Nawatakia maandalizi mema ya Sabato

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa Sasa Dar es salaam
 
Umezunguka sana na maelezo yako ila kwa kifupi ili mtu kufanikiwa au kutofanikiwa zipo njia mbili tu ni
Ufate nguvu ya Nuru au giza.

Njia ya Nuru ina sheria zake pia njia ya giza ina taratibu zake.
Lakini pia ukifata njia ya Nuru au giza pia kuna sheria ndogo nyingi sana zakufuata ili mtu afanikiwe.
 
"You become what you Think"

Mtu anaanza kua tajiri kabla hajawa Tajiri, Agano ni moja tu "Nataka kua fulani" , Then unaachana kabisa na vitavyo kukwamisha kufikia pale, its over..

Ukishakua na nia, Ukaishinda hofu ya kufeli, ukawa high motivated, Ukawa na msimamo, Ukawa mtu usie kata tamaa its over, Yo're unstopabble!!

👇👇👇 Msikilize Denzel Newton, pitia na hicho kitabu;
 
Attachments

Hapo ndipo mafanikio huanzia kabla ya wengine kuyaona

Umeelezea kitu kikubwa sana ambacho wengi hawana uelewa nacho

Nyumba, Pesa, Magari na mengine tunayoyaona kwa macho ni matokeo tu.

Mtu kufanikiwa kunaanzia katika Misingi hiyo uliyoeleza.
 
Atimae p diddy na washkaji zake wamefikiwa na Mtibeli.
 
Hapo ndipo mafanikio huanzia kabla ya wengine kuyaona

Umeelezea kitu kikubwa sana ambacho wengi hawana uelewa nacho

Nyumba, Pesa, Magari na mengine tunayoyaona kwa macho ni matokeo tu.

Mtu kufanikiwa kunaanzia katika Misingi hiyo uliyoeleza.

Kweli Kabisa
 
Mtibeli andiko lako ni zuri sana ,ila kidogo linatuacha wasomaji juujuu ikikupendeza ingia deep kidogo mtibeli
 
KIAPO NA MAAGANO YA KUFANIKIWA KATIKA MAISHA.

Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli

Hii ni Moja ya zile Siri ambazo nilikuahidi nitakueleza. Na lolote nitakalokuahidi nitatimiza. Wala sitasahau kutimiza lolote nililokuahidi.

Haya nisikie Sasa,

Mafanikio yapo ya aina mbalimbali. Kîla Mtu anahitaji kufanikiwa katika Yale anayoyapenda. Wàpo wanaohitaji mafanikio ya kielimu, Wengine mafanikio ya Kifedha, Wengine mafanikio ya kindoa na familia, Wengine mafanikio ya kitaaluma, wengine umaarufu miongoni mwa mambo mengine.

Sasa ili ufanikiwe katika Jambo lolote au mambo kadhaa kuna Kanuni na njia ambazo lazima uzijue na kuzipitia.

MAFANIKIO YANAHITAJI MAMBO MAKUU MATANO.
1. NIA na Kupenda
2. Ujuzi na maarifa.
3. Viapo na MAAGANO.
4. Wakati/Muda.
5. Watu na mazîngira

Mambo manne Hapo juu ni maarufu Sana. Lakini Jambo Moja àmbalo ni VIAPO na MAAGANO kwèñye mafanikio siô maarufu Kwa Watu wengi na haisemwi semwi.

Hakunaga mafanikio Bila KIAPO na MAAGANO. Hayo mafanikio hayapo.
Huwezi kufanikiwa Kwa lolote Bila ya Kiapo au MAAGANO

MAAGANO NI NINI?
Maagano ni Makubaliano, Mkataba ambao wahusika wawili au zaidi huingia katika kushirikiana au kufanya Kazi pàmoja katika kufanikisha Jambo Fulani.
Katika Mkataba au agano kunakuwa na vipengele àmbavyo wahusika wanakubaliana kuvifuata ili kushirikiana katika kutimiza au kufanikisha Jambo Fulani.

Hivyo Mkataba au maagano hulenga kufanikisha Jambo Fulani. Hii NI kusema Hakuna mafanikio Bila MAAGANO, makubaliano au Mkataba.

Katika Mkataba kûna wahusika Wawili;
1. KIONGOZI, BOSS, BWANA, MIUNGU, MTAWALA, AU MHUSIKA YOYOTE AMBAYE NDIYE MWENYE POWER NA AUTHORITY

2. MTUMISHI, MWAJIRIWA, MTU au kiumbe, au MHUSIKA yeyote àmbaye NI mhitaji na asiye na Ñguvu.

Jambo Moja kubwa kwèñye MAAGANO au Mkataba NI kuwa kîla MHUSIKA anakuwa na Jambo lake àmbalo anataka lifanywe na MHUSIKA Mwingine. Ingawaje mtawala au Yule mwenye Ñguvu ndiye mwenye Ñguvu zaidi katika Mkataba huo wa Kutoa maelekezo zaidi yakufuatwa.

Mfano, Mtu anahitaji kuwa tajiri, anaweza kuwa na vigezo vyote Kabisa kama Nia na Mapenzi ya Kazi Fulani àmbayo itampatia utajiri, Elimu na ujuzi wa kumpatia utajiri, mazîngira, lakini atakosa mambo Makubwa mawili àmbayo ni Watu au wahusika Sahihi na Wakati Sahihi na Hapa ñdipo Lazima aone umuhimu wa kutafuta weñye Ñguvu na Mamlaka àmbao ataingia maagano n Kula viapo nao ili wahusika hao wampatie Watu pàmoja na mûda Sahihi mzuri wa kufanikiwa.

Kîla unayemuona Hapa Duniani yupo chini ya Mamlaka na falme Fulani.
Kama ilivyo kîla Mtu unayemuona yupo chini ya Tawala Fulani. Kuna watañzania, Wakenya, waingereza, wafaransa n.k.

Ili Muingereza ashirikiane na Mtanzania lazima yawepo Makubaliano na mikataba Kati ya Taífa la Uingereza na Tanzania.

Muingereza hawezi kûja kuchuma Mali Hapa Tanzania Bila kupewa KIBALI na serikali ya Tanzania. Na akifanya kinyume akikamatwa hunyang'anywa zile Mali na kufunguliwa Mashtaka ya kijinai.

Baàda ya Mtu kuwa na NIA na Kupenda Jambo Fulani na unalihitaji itakupasa úwe na Elimu (ujuzi na maarifa) Kwa Jambo lenyewe. Kisha uyajue mazîngira na namna ya kuishi Katika mazîngira ya Kile unachohitaji. Mazîngira ni pàmoja na Watu lakini Watu ni hoja inayojitegemea.

NI lazima uchague utaingia makubaliano na Mamlaka au Tawala Ipi ili uweze kufanikiwa. Lazima usome Mkataba uuelewe Kisha ñdipo Ule KIAPO.

KIAPO!
Kiapo ni Sahihi inayotolewa na Mtu au Watu wanapoingia Makubaliano. Kiapo ni kuji-commit. Kujifunga. Lakini pia Kiapo ni uthibitisho kuwa umekubaliana na yaliyomo kwèñye Mkataba au agano lenu.
Kiapo ni approvement.

Sasa shirika au Kampuni au falme utakayoingia nayo makubaliano ndiyo itakayokufanikisha Kwa sababu utatumia Resources zote zilizopo kwèñye ufalme Husika.

Resources zilizopo ni kama Ifuatavyo;
1. WATU.
Rasilimali Watu ni Moja ya nyenzo muhimu ili ufanikiwe.
Falme uliyoingia nayo makubaliano ndiyo itaratibu wahusika wôte watakaokusaidia kufanikiwa. Kwa sababu Huwezi kufanikiwa Bila Watu. Na Huwezi kuanguka Bila Watu

Hivyo ufalme utakukutanisha na wahusika Kulingana na mipango na Wakati Sahihi kadiri ufalme utakavyokuwa umepanga.

Jambo Moja la uhakika NI kuwa, Adui zako watakuwa Adui za ufalme na Adui za ufalme ulioingia nao Mkataba watakuwa Adui zako.

2. WAKATI(MUDA) AU RATIBA.
Ratiba za màtukio vitakuwa vinaratibiwa na Mwajiri wako. Lini na Wapi úwe hiyo haitakuwa juu yako. Wakati gàni utakutana na Nani hiyo haitakuwa juu yako.
Unapoajiriwa Mamlaka ndîo hukuwekea RATIBA zîpo Ratiba za wazi Ambazo utakuwa unazijua na zîpo Ratiba za Siri ambazo hizi Mamlaka ndîo huwa zinajua zenyewe.

3.VITENDEA KAZI.
Vitendea Kazi vyote utakuwa unapewa lakini kîla Jambo litafanyika kiprotokali. Yaani kîla Jambo litaenda kiutaratibu Kwa kuzingatia Sheria na makubaliano ya agano lenu.

Watu wengi wanaweza wasielewe Jambo hili lakini ndivyo lilivyo.

MTU unaweza kufungua biashara hata pale Kariakoo kwèñye maelfu ya wateja lakini ukafunga Kwa kukosa wateja Wakati Jirani yako anafanya biashara hiyohiyo yeye anafanikiwa.
Tenà mtaji unaweza Ukawa Mkubwa kuliko na Kazi Ukawa unafanya vizuri kuliko Jirani yako lakini wateja wakamfuata Jirani yako

Unaweza Ukawa na kipaji chakuimba kuliko hata Diamond Platinum na wengi tunawaona wanakila kitu kumzidi Diamond Platinum kuanzia sauti nzuri, nashauri, mwonekano mzuri lakini wameshindwa kwèñye Game ya Muziki.

Wakati nasoma, kûna Watu walikuwa vichwa na walikuwa wanafanya vizuri lakini kwèñye mtihani wa mwisho waliangukia pua Wakati huohuo Wengine àmbao hawakutarajiwa wakaibuka.

Kûna Mtu anaweza akasema wekeza kwèñye Mitandao au masuala ya Tehama mfano kuanzia mitañdao kama Facebook, sijui Tiktok sijui Instagram.
Kwa wasiojua NI kuwa kûna Mitandao ya kijamii kama Facebook au tiktok mamia yanayokaribia maelfu lakini why Facebook na Tiktok inakimbiza?

MTU anaweza kufanikiwa kwèñye Maisha na akashindwa kusaidia ndugu Zake Kwa sababu ndugu Zake hawapo kwèñye chain ya Mamlaka aliyoingia nayo Mkataba au maagano.
Mbaya zaidi unaweza ukashangaa MTU kasaini Mkataba na falme shindani na falme ya Wazazi wake. Hapa Wazazi lazima waone mbona Mtoto hatuletei Pesa.

Mfano, Mzazi anaweza kuwa yupo kwèñye falme za kichawi au Mizimu Wakati Mtoto yupo kwèñye falme za Mungu Muumbaji. Automatically Mtoto hata akifanikiwa atajikuta hawezi kusaidia Wazazi wake Kwa sababu wàpo falme Mbili tofauti.

Au Mzazi kafanikiwa na nitajiri yeye agano amefanya na Mizimu au Wachawi lakini Watoto walipokuwa Hawakukubali kusajiliwa kwèñye agano la Wazazi. Hiyo utashangaa Mali zinaishia Kwa Wazazi na kupotea.

Kuvunja Baadhi ya vipengele katika Mkataba au agano hupelekea Mtu kupata adhabu Fulani ikiwezekana kuangamizwa.

Mathalani, Mtu anapotumia Mali au Rasilimali za ufalme au Kampuni Kwa Watu wasio WA Kampuni, hasa Kampuni au ufalme shindani hii huweza kupelekea kufilisika au kuangamizwa Kabisa.

Ndîo maana kwèñye familia NI muhimu Watu Kuoa na kuolewa na Watu weñye Imani Moja na àmbao watatumika Kwa Mfalme au utawala mmoja.
Kumsaidia tuu Mke au Mume àmbaye yupo opposite na Mahali ulipofanya agano NI Kutengeneza mazîngira ya kufilisika, kufukuzwa Kazi, kuanguka kimaisha.

Kusoma kwako siô lolote
Kufanya Kazi Kwa bidii siô lolote.
Nia na Kupenda Jambo Fulani siô lolote.

Kwa Mfano hata Jamiiforum unaweza Ukawa unasoma mambo mbalimbali lakini kama siô Member wa Jamiiforum kûna fursa hutozipata kama Kutoa maonî yako, kushiriki Baadhi ya fursa zinazohusu member

Na ili úwe kwèñye mtandao Fulani lazima usaini na Ule kiapo kuwa utafuata terms and conditions za JF.

Acha nipumzike sasa

Nawatakia maandalizi mema ya Sabato

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa Sasa Dar es salaam
Hii ni kubwa Sana.
 
Back
Top Bottom