Kiasi cha kodi TRA Tafadhali...

SWEEPER

JF-Expert Member
Joined
Jul 16, 2012
Posts
269
Reaction score
87
Nataka kununua gari aina ya Toyota Gaia ya mwaka 2001 ipo Dar es Salaam showroom bei US$ 3950 haijalipiwa kodi. Kwa wanaofahamu naomba kiasi cha kodi nitakachotakiwa kulipia TRA.
 
Mkuu mbona jazba???
NHC kazi yao nini mkuu? Acha kasumba za kimaskini kufikiri nyumba ndo mafanikio ktk maisha. Nina nyumba ya vyumba 4 kimara, ninaishi nyumba ya kupanga magomeni. Nisaidie nilichouliza.
 
Kaka Sweeper makisio ya ushuru wako sijayajua vizuri maana sijajua gari yako ina cc ngapi maana hiyo pia ni muhimu ktk hesabu za tra,so ukiweza leta chasis number yako ili upate hesabu nzuri...lakini kwa maelezo machache uliyotoa ni kwamba kwa tra peke yake andaa 5.5ml maana gari lako lina dumping fee maana limezidisha miaka 10 na cif yake ni $3950..pia wawezatembelea website hii itakupa makisio gariyangu.com nakutakia mafanikio...siku hizi tax za tra zipo juu sana kuagiza vitz au ist ya mwaka 2004 ni lazima uwe na 3.5ml ili kufanya clearance za tra na port!!!+971504374387 dubai
 
Kwa aina hiyo ya Gari, TRA wataithaminisha kuwa ilipokuwa mpya bei ilikuwa US$ 24,500
Wakiondoa profit margin na kulidepreciate kwa sasa litakuwa na thamani ya US$ 2,624.05.
sasa utalipa vifuatavyo ndugu:-

Import Duty US$ 656.01
Exc Duty (cc) 164.00
Exc Duty ( Damp Fee) 656.01
VAT 738.01
Julma(Duties & VAT) US$ 2,214.03

Hesabu hiyo hapo na kwa msaada zaidi tembelea www.tra.go.tz na pia kujua equivalent
TZS itategemea exchange rate ya siku ya kulipa kodi. Pia watakiwa na kuwa sio chini ya
laki tano kwa mambo mengine kama fire, port charges n.k

CIA

N:B

Nauza RAV 4 ya 2004 in case u
 
Hivi hizi bei za TRA za Magari yalipokua mapya wanazipata wapi. Mimi nina mashaka nazo sana!

Kwa mfano tuangalie bei zifuatazo za Toyta RAV4


Model Year CC Price
RAV 4 ZCA26W 5 - DOOR ≤ 2003 1800 60,111
RAV 4 ZCA26W 5 - DOOR 2004 1800 53,432
RAV 4 ZCA26W 5 - DOOR 2005 1800 51,206
RAV4 ZCA 3-DOOR 2000 1800 50,379
RAV4 ZCA 3-DOOR 2001 1800 57,149
RAV4 ZCA 3-DOOR 2002 1800 59,825
RAV4 ZCA 3-DOOR 2003 1800 59,825
RAV4 ZCA 3-DOOR 2004 1800 45,481
RAV4 ZCA 3-DOOR 2005 1800 40,932

source TRA


Fananisha bei hizo na bei ya Toyota RAV4 GX 5D Wagon 2013 - $23,300

source: Toyota Rav4 2013 | Crossover SUV


Jamaa wanakisia Ama?
 
Tra uwa hawana bei zinazoeleweka ata kidogo kuna kipindi niliagiza gari ushuru ukaja kama 4.8ml baada ya kupewa bei hiyo nilikwenda mwenyewe kwa meneja wa masuala ya tax pale TRA baada ya kuongea naye bila kutoa chochote ushuru ulishuka mpaka 3ml nilishangaa sana !!! Pale ni maelewano hawana formular inayoeleweka katika kutoza ushuru
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…