Kiasili Binadamu hapendi Uhuru lakini anauogopa Uhuru

Kiasili Binadamu hapendi Uhuru lakini anauogopa Uhuru

Pile F

Senior Member
Joined
Aug 15, 2020
Posts
121
Reaction score
170
Habari ya leo wanajamvi. Ninatoa Pole na hongera mnapofanya kazi zenu kwa jitihada kubwa. Mola awajaalie mema yazidi kuongezeka. Moja kwa moja ninawakaribisha kwenye Mada:

Katika mtazamo wa kwanza jambo hili huonekana kuwa si kweli. Tangu wakati wa Plato kumekuwepo na mawazo kuwa Binadamu siku zote anatafuta Uhuru lakini umezuiliwa na Ulimwengu wa Uadui.

Binadamu hupenda kujifikiria kama roho jasiri zinazopigania kuwa huru katika uso wa Ulimwengu ambao unawapinga na hata kuwatatiza. Lakini ukweli upo tofauti kabisa; hatuupendi uhuru lakini tunauogopa.

Kama tunavyojaribu kuelewa juu ya kuinuka na kuanguka kwa Ustaarabu katika historia ya wanadamu, tunaweza kuona kitu cha huu muundo kinachosababisha ‘Kushindwa kwa Ujasiri’ ambacho kinaonekana kuwa kitangulizi cha kupungua au kupotea kabisa kwa jamii fulani zilizowahi kufahamika.

Kutokana na mtazamo huu, historia ya wanadamu inaonekana kuwa ‘Si mapambano ya Mwanadamu kupata Uhuru kutoka kwenye ulimwengu unaotatiza jitihada zake; lakini ni rekodi ya Upotofu au Utoro ambao binadamu anatafuta ili kuuepuka Uhuru ambao ulimwengu humpatia pasipo majuto juu yake.'

Kuukubali uwajibikaji huambatanisha kuuondoa usalama wa kile tunachokijua na kukielewa na hivyo kuchukua uamuzi wa ajabu, ambao ni kukubali uwajibikaji kwa ajili yetu sisi wenyewe.

Muumba wa Mbingu na Ardhi na Wanadamu anamwambia Mtume Muhammad na kusema katika Quran 14:1 “Kitabu tumekiteremsha kwako ili uwatoe watu kutoka gizani kwenda kwenye nuru”.

Hivyo basi mfumo wa Uislamu ambao chimbuko lake ni kitabu kitakatifu cha Quran umekuja kumkomboa mwanadamu kutoka katika Utumwa wa kila aina na kumfungua minyororo yote iliyomzonga.

Kimemkomboa Binadamu kutoka katika utumwa wa kiitikadi wa binadamu kuabudu vitu vya kushikika au mawazo na fikra za binadamu mwenziwe na kunyanyua heshima yake na Utu wake juu ya kila kitu duniani kwa sifa yake kama binadamu.

Ndiyo maana Yesu pia, kusudi apate kuwatakasa watu, kwa damu yake mwenyewe, aliteswa na kufa nje ya mji. Basi, tumwendee huko nje ya kambi tukajitwike laana yake. Maana hapa duniani hatuna mji wa kudumu; lakini tunautafuta ule unaokuja. (Waebrania 13:12-14)

Ni safari ya gharama haswa na kubwa kuuendea Uhuru. Swali, Je, Wanadamu tunaweza kuifanya hii safari?

Hapa, nataka kusema, jambo alilozungumza rafiki yangu juu ya Kuibuka Upya kwa Ukabila Afrika ya Mashariki.

Maoni yake yalikuwa, kama nilivyoyaelewa, kuwa kama ongezeko la kiwango cha uzoefu wa binadamu juu ya ulimwengu haliambatani na uelewa wa kidini ambao una uwezo wa kuumba dunia mpya katika mazingira ya kibinafsi ‘kunakuja kukataa kwa sehemu ya wengi majukumu ya Uhuru;

Kuondoka kwa usalama wa kufikirika wa maisha ya kikabila, ni usisitizwaji kwa mara nyingine juu ya Utegemezi wa mwanadamu kwenye nguvu za asili zisizo za kawaida.'

Je, ni kuchanganyikiwa kwa ufahamu wetu pale hali hii inapoleta Uchungu na Kilio kuwa Utume wa Kikristo au Uislamu umeharibu tamaduni za kiafrika?

Kama ni hivyo, kushindwa kwa hizi tamaduni hakupo sana kwenye kuwa ziliharibiwa, kama vile ilivyo kwenye namna ambavyo tamaduni hizi hazikubatizwa kwa Waafrika wenyewe, wakati ambapo ubatizo ulikuwa unawezekana; kuwa ukombozi wa akili ambao Ukristo na Uislamu ulileta kwa kiwango fulani ulikuwa hauongozani na ukombozi wa kulinganishwa wa Uelewa na Hisia kwa ujumla.

Hofu ni adui mkubwa wa Uhuru wa mwanadamu na hujieleza yenyewe pale inapoondolewa au kwenye majaribio ya kuleta Ubwana juu ya wengine.

Wakati hofu inapotawala, nafsi ni kitovu cha kumbukumbu, na hata kama tutachuchumaa na kuinama katika gereza letu au kuling’ang’ania, na kuliita Kikoa au Himaya yetu, gereza ni lenyewe na litaendelea kuwa gereza, mpaka Upendo uitupilie nje hofu na tutakuwa tumefunguliwa na kuwa Huru.
 
Asante Numbisa na chuma cha mjerumani kwa tafakuri

Lakini tuwe wazi kuwa katika kuzungumzia Uhuru hatujaribu kumaanisha nguvu ya kufanya kile ambacho kimaumbile hakiwezekani.

Mtu anayejaribu kuruka kutoka kwenye mnara ataanguka chini na hatakwenda juu, na hayupo huru kuchagua kufanya kimojawapo kati ya harakati hizo mbili.
 
Back
Top Bottom