Kiba akwama kwa saa kadhaa Uwanja wa Ndege Kotonou

Mphamvu

JF-Expert Member
Joined
Jan 28, 2011
Posts
10,702
Reaction score
3,319
Msanii wa Bongo Fleva, Ali Kiba, juzi alikwama kwenye Uwanja wa Ndege wa Kotonou, Benin kutokana na ndege yao kutua kwa dharura kwa kilichodhaniwa kuwa ni hitilafu kwenye mfumo wa hewa wa ndege hiyo.

Nguli huyo wa Muziki mwenye zaidi ya Miaka 10 kwenye muziki alikwama alipokuwa akirejea nyumbani akitokea nchini Naijeria kutumbuiza kwenye tuzo za AMVCA, ambako Watanzania wawili, Lulu Elizabeth Michael na Single Mtambalike walipata tuzo.

Msanii huyo pamoja na abiria wengine walikaa hapo kwa zaidi ya masaa mawili kabla ya safari yao kuendelea. Mastaa waliokuwa na King Kiba kwenye safari hiyo ni pamoja na Salvador, mchekeshaji wa Uganda, Sharon Mundia, Bloga wa Fasheni kutoka Kenya na Robert Burale, mchambuzi wa masuala ya fasheni.


Chanzo: Standard Media
 
vipi ameshafika lakn, au ndo kaenda kupga selfie akiwa nchi nyingine wakati wenzake wanawaza mbinu za kujaza account.
Hata kupiga kwake mswaki mtaponda... Pole Mzee kiba ndo huyo katoka kupiga hela unaponda kizeeembe
 
mashabiki wa wema ndo wanampaisha kiba,ila mashabiki.wa.wafanya vizuri wapo na chibu dangote the special one
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…