Kibadeni in Action: Kili Stars 4-0 Somalia

Kibadeni in Action: Kili Stars 4-0 Somalia

Makoye Matale

JF-Expert Member
Joined
May 2, 2011
Posts
6,491
Reaction score
2,104
Huku familia ya wanasoka nchini Tanzania ikiwa katika maombolezo ya Taifa Stars kupigwa kipigo cha karne cha 7-0 na Algeria, timu ya Tanzania Bara (Kilimanjaro Stars) imeanza kupoza machungu ya maombolezo hayo baada ya muda mfupi uliopita kuifumua Somalia kwa bao 4-0. Magoli ya Kili Stars yamefungwa na John Bocco (11' na 56') na Elius Maguri (17' na 53').

Kilimanjaro Stars XI to face Somalia today 22/11/2015
Aishi Manula,
Shomari Kapombe,
Mohamed Hussein,
Salim Mbonde,
Kelvin Yondani,
Himid Mao,
Saimon Msuva,
Said Ndemla,
John Bocco,
Elias Maguri,
Deus Kaseke.

Sub's:
Ally Mustafa,
Kessy Ramadhani,
Hassan Isihaka,
Jonas Mkude,
Salum Telela,
Salum Abubakar,
Malimi Busungu

Source: https://twitter.com/Tanfootball

Asante sana Mzee Kibadeni, keep it up!
 
somalia kuna ligi????

alishabab walishakataza ligi nchini.somalia..na ukicheza shart uvae suruali no bukta
 
Hivi wale wa TP Mazembe hapa hawahusiki?

Wanahusika wala hawazuiliwi kucheza mashindano haya, tatizo ni kuwaharibia nomino zao pindi tunapocharazwa kipigo kama cha 7-0. Ni busara ya Kibadeni kuwaacha waendelee na maandalizi ya Klabu Bingwa ya Dunia.
 
Haahaahaaa! !!! Kuifunga somalia ndio tunajidai sasa. Haahaahaaa.!!!!
 
Wanahusika wala hawazuiliwi kucheza mashindano haya, tatizo ni kuwaharibia nomino zao pindi tunapocharazwa kipigo kama cha 7-0. Ni busara ya Kibadeni kuwaacha waendelee na maandalizi ya Klabu Bingwa ya Dunia.

Ok...hope waliochanguliwa hawatatuangusha...
 
Wazee wa saba wamepiga mtu

Naomba niweke sawa kumbukumbu:

Timu iliyopigwa 7-0 na Algeria ni timu ya Tanzania iitwayo Taifa Stars, kocha wake ni Boniface Mkwasa.
Timu iliyoipiga Somalia 4-0 ni timu ya Tanzania Bara iitwayo Kilimanjaro Stars, kocha wake ni Abdallah Kibadeni.
 
Si miaka mingi tutamtwanga huyo kenge(algeria) mpaka utamkana kwa ulimi wako. Note my word mkuu.

Miaka 5 tu tunamgonga huyo mtu.

Mkuu yakitimia hayo nitakuwa ni mtu mwenye furaha kuliko wewe maana baada ya kile kichapo kukishuhudia kwa macho yangu sikuweza kupata usingizi wa maana kwa muda wa siku 3 mfululizo, kila nikilala nilikuwa nawaona Barthez na Manula wakiokota mipira nyuma ya goli letu. Tangu nimezaliwa nilikuwa sijakutana na kipigo cha 7-0 kwa timu ninayoipenda na ninayoishabikia. Mikia walipotupiga 5-0 walijidai sana kumbe kuna wanaume wanpiga 7-0!
 
Back
Top Bottom