Kibaigwa; Muokoeni mtoto Filemon anayeteswa na mama yake

Kibaigwa; Muokoeni mtoto Filemon anayeteswa na mama yake

Trainee

JF-Expert Member
Joined
Sep 22, 2018
Posts
2,660
Reaction score
3,501
Huyu mtoto anaishi na MAMA YAKE MZAZI pale Kibaigwa sehemu inaitwa Mbagala, anasoma chekechea. Mama huyo anamtesa sana mtoto huyo na haambiliki hata kwa mbali mpaka majirani wameamua kuwa wakimya na kubaki kuangalia tu jinsi mtoto huyo anavyoteswa. Wanasema mama huyo ana 'mdomo mchafu' sana pindi utakapojaribu kumuonya/ kumsihi juu ya unyanyasaji wake kwa mwanaye.

Habari kwa ufupi...

Baba na mama Filemon wana watoto wawili yaani Filemon na mdogo wake mdogo zaidi. Walikuwa wakiishi Morogoro mara huyu mwanamke akamshauri mumewe wakajenge Kibaigwa.

Baada ya kujenga mwanamke akaja kukaa hapo na akakataa kabisa kurudi Moro. Maelezo mengine hapo ni marefu ila kwa ujumla baada ya kuanza kuishi mwenyewe hapo ndipo mateso kwa mtoto yalipoanza nataja mifano kadhaa.

Chakula mama anapika kutwa mara moja yaani kama ni saa kumi jioni ugali basi mpaka kesho saa kumi jioni tena ndipo wale halafu siyo kwamba hakuna chakula ndani, laa! Hakuna shida kihivyo ya kuwafanya wale mlo mmoja.

Akianza kumpiga anapiga kama sio mtoto tena kosa lenyewe unakuta ni limetokana na yeye mwenyewe mama.

Kubwa kuliko ni hivi juzi sasa wakati napita hapo mpaka kupewa mikasa yote hiyo. Ni kwamba dogo alishutumiwa ameiba hela ndani aisee akapigwa kisha akakamatwa mkono na kuingizwa kwenye kama siyo majivu ya moto basi mafuta ya moto akaungua mkono.

Majirani wanahisi ni mafuta kwa sababu inaonesha amechomwa mkono wa kwanza kisha kutaka kuchomwa wa pili akacholopoka akakimbia ila katika kukung'uta mkono basi mafuta yakarukia na matone matone kudondokea mkono wa pili nao ukapata majeraha kadhaa.

Binafsi niliwashauri majirani hao washtaki kwenye ofisi yoyote ya serikali iliyopo karibu lakini walionesha kutokujua lolote kuhusu ofisi hizo.
 
Nilishauri hivyo chifu baada ya majirani kusema hawazijui ofisi za serikali
Mkuu nikuombe sana nenda mwenyewe kituo cha polisi waeleze habari kamili uambatane nao hadi kwa huyo mama na bahati nzuri majirani watakuwa mashuhuda wazuri.

Mtoto hawezi kujitetea mwenyewe bali watu wazima ndo watetezi wao. Usipofanya hivyo huyo mtoto akiendelea kuteseka nawewe utakuwa kwenye mnyororo wa dhambi hiyo.

Inauma sana. Kwasababu nipo mbali tu kikazi otherwise ningekuwa nyumbani ningekuja hapo Kibaigwa kumalizana na huyo mama kisheria ili iwe fundisho kwa wajinga wengine.

Ningekuwa vizuri kwa muda huu ningekutumia hata hela kidogo ya kutwa ili uache shughuli zako ufuatilie jambo hili polisi.
 
Mkuu jitolee UENDE polisi dawati la jinsia kwani huyo ni mtoto wetu sote.Mimi Binafsi nimefanya hivyo mara nyingi na MOYO WANGU huwa unahama ninaposikia haki ya mtoto inachezewa. Pia kama uko jirani na halmashauri nenda kamwone afisa ustawi wa jamii mweleze yote atachukua hatua.
 
Nimewaza kitu kimoja.... Jamii inayomzunguka mtoto inachohofia ni mdomo (matusi) kutoka kwa muhusika tu au kuna kingine?

Ni vyema jamii ikawaza zaidi ya kutoa taarifa, ikiwezekana wamchukue au waonane na mashirika pindi mtoto anapoonekana ndio chance ya kumchukua au kuwa chukua na kuwaondoa eneo Hilo kisha hatua nyingine zitafuata nikiwa na maana hatua za kupata maelezo kutoka kwa mama zitachukuliwa tu baada ya watoto kuwa sehemu salama...

Neno la mwisho kwetu hasa jamii hasa sisi tunaovaa suruali (wanaume)

Tujifunze kutunza na kutimiza wajibu wetu kama tunavyokuwa tayari kwenda kutoa mbegu zetu kwa hiari yetu, hawa wanawake suala la kuwanyanyasa watoto mara nyingi ukiwafuatilia utagundua sisi wanaume ni moja ya chanzo hicho


Asante....
 
Wanawake km hao sio wazima aisee aidha huwa na msongo wa mawazo, matatizo ya akili na hapa ndo kwenye tatizo akiwa na hasira hajimudu na wako wengi wenye Tabia hizo hafai kuishi peke yake mm huwa nashangaa Kwa kweli roho mbaya Kwa mtoto wako ina faida gani, inakupeleka wapi hakuna Faraja nzuri km kuwa na mtoto sijui shida inakuja wapi Ila hao majirani sio kabisa na naniwajinga kupindukia.

Kuna mpangaji mwenzangu Alikuwa ana mke km huyo ukimkwaza ama akikerwa huwa na hasira na Jamaa huwa anawaondoa watoto wote kwenye nyumba akishika kitu harudishi kiwe cha hatari kisiwe cha hatari anadhuru ni Chizi fresh anaetembea pasipo kujijua pale anaposhikwa na hasira.

Kuna siku nilikuwa napita Gongolamboto sokoni kuna mama mmoja nimfanya biashara ndogondogo akawa anampiga mwanae ni mtoto wa miaka minne anampiga km anapigana na MTU mzima mara mateke, ngumi na haangalii pakumpiga unajua wafanya biashara wenzie walimfanya nini walianza kumchapa makofi Yule mama ya nguvu mwisho Yule mtoto akawa anamuombea mama Ake Jamani msipige mama yangu wakaacha. Huyo anatakiwa adaabishwe au akae na MTU kama mumewe sio peke yake ni mgonjwa asie jijua anaepelekeshwa na hasira anapoudhiwa.
 
Mkuu nakuomba timiza wajibu wako kwa kusaidia kufikisha taarifa za unyanyasaji wa huyo mtoto kwa serikali ya mtaa husika au polisi.
Jukumu la kuhakikisha watoto wanalelewa kistaarabu ni la jamii nzima kwa kuwa akiachwa akaishi katika ukatili huo baadae atakuwa na roho na tabia za ajabu ambazo zinaweza hatarishi kwa jamii nzima,kwako, kwangu au kwa watoto wetu.
Tabia nyingi mbaya tuzionazo au tufanyiwazo na watu tusiowajua ama tunaowajua ni matokeo ya jamii kupuuza matukio kama haya.
 
Huwa sivumilii ujinga kama huu nikiuona.Ungeenda police mkuu,msaidieni mtoto jamani.Wanaumizwa sn watoto huko majumbani
 
Back
Top Bottom