Herbalist Dr MziziMkavu
JF-Expert Member
- Feb 3, 2009
- 42,872
- 34,363
Last edited by a moderator:
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Nchi imeoza kuanzia kwa president mpaka kwa walinda usalama hapo vituoni ukimpeleka kituoni siku mbili unamkuta mtaani na atakuumiza wewe.Kama mkasa ulionikuta nilivyotembelea sehemu fulani kipindi niko vacancy.Kwa mimi nasapoti kama ameshikwa na ushahidi iwe tit for tat na yeye anapewa kichapo cha paka mwizi.Na ikiwezekana ni kumtoa roho ili iwe fundisho kwa wengine wenye tabia kama hizo
Sasa ndugu yangu kama mimi ambaye nilikwenda nyumbani siku moja nikaamua kusimamia biashara yangu mwenyewe ya daladala na kuishia kukabwa na vibaka pale Victoria nitaachaje kusuport mob psychology wakati mwizi wangu ninamuona anatokomea na pesa yangu?Hapo pekundu ndio kwenye shida katika issue za mob justice. Ndio maana watuhumiwa wanatakiwa kupelekwa mahakamani - katika hali nyingi kama ilivyosemwa na wadau watu huuawa na baadaye ushahidi huonyesha kwamba hawakuwa majambazi.
Nakumbuka kwa huzuni tukio moja la Mabibo miaka kadhaa iliyopita. Bwana moja akiitwa Gonelimali aliingiliwa na majambazi usiku, akapiga kelele kuomba msaada. Watu waliitikia lakini wakamwua mwenyewe. Alikuwa ametoka nje kufuatilia majambazi akawa katika migomba iliyo around nyumba yake. Maskini akadhaniwa ndiye jambazi. Kelele za kujitambulisha hazikusaidia. "Mob justice!"
Sasa ndugu yangu kama mimi ambaye nilikwenda nyumbani siku moja nikaamua kusimamia biashara yangu mwenyewe ya daladala na kuishia kukabwa na vibaka pale Victoria nitaachaje kusuport mob psychology wakati mwizi wangu ninamuona anatokomea na pesa yangu?
Ndugu umenikumbusha : Nina visa viwili navyo fanana na hiki: tulikuwa natabia ya kuacha pipa nje kutokana na ukame wa maji hasa kipindi cha mvua ili kama mvua ikinyesha niwe nauhakika wakupata maji, likaja kuibiwa pipa nilikasilika sana, baada ya siku mbili, jirani yetu alikuja kuniamsha mida ya saa 12 asubuhi, akanieleza kuna mtu kalala kwenye kibanda chetu ambacho kilikuwa kama mita 30 kutoka kwenye nyumba yetu, lakini huyo jamaa alielala humo anapanga na kisu pembeni haraka haraka nikaamka nikavaa nikachukua wire ambao huwa wanatumia kufungia baskeli tukaenda kwenye kile kibanda tukamkuta jamaa amelala mpaka nakoloma, tukafungua kipanda tukazichukua panga na kisu, ndiyo tukaanza kumpiga huku tukiita mwizi watu walijaa kila aliyekuja alitusaidia kumtwanga daah jamaa tulimpiga ile mbaya, akaja balozi akatutaka tumpeleke polisi kabla hatuja mpeleka polisi akatokea jamaa ambae anakaa mtaa ulele akatuambia huyu jamaa walikunywa nae pombe mpaka saa 10 usiku kwenye baa moja ambayo iko maeneo hayo hayo naalikuwa amelewa sana, ndipo watu wakaanza kumhoji yeye ni nani ametokea wapi, jamaa alisema yeye ni fundi ujenzi kuna site anajenga jana yake akuwa kwenye baa iliyotajwa maka usiku…alikuja kwenye kile kibanda baada ya kulewa na kuishiwa na ilikuwa usiku sana ndipo alipo amua kuingia kwenye hicho kibanda na panga na kisu sio vyake, ndipo watu wakaamua kumfaata mwenye kibanda(mpangaji wakibanda) akavitambu panga na kisu kuwa ni vyake, nilicholopoka kwenda nyumbani maana nilijua sasa kibano kinatugeukia baadae jamaa aliombwa na balozi atusamehe naakapewa Tshs 20000 akatibiwe…baada ya miezi mitano kupita nilikumbana na kisa cha pili: Nilienda kwa rafiki yangu baada ya miezi mitatu bila kwenda kwake....kisa kilianza baada ya kufika mahali hapo nilikuta akina mama wanasukana sikuto salaam nikaingia ndani nikimwita shemeji yangu maana nilikuwa na utani nae kilicho nishangaza nilikuta kila nilicho kiona kilikuwa kigeni kwangu, nyumba yenyewe ilikuwa ni chumba na sebule nilipo angalia chumbani liona mpaka viatu mashuka tofauti nikashituka nikatoka nje kumbe wale akina mama wananisubilia nje na mbaya zaidi majuzi yake waliibiwa, ile natoka wakaita mwizi mwizii mwizi mwizi nikajua nimekwisha watu wakaja bahati nzuri watu wa kwanza kuja walikuja watu ambao wananifahamu na nusu saa iliyopita nilikuwa nasheza nao mpira...wakanipa nafasi ya kujieleza ndiyo watu walipo gundua mimi siyo mwizi na kosa nililofanya ni kuta wasalimia wale akina mama kwani wangeweza kuniuliza naenda wapi... kabla hata sijaingia ndani...Haya mambo bwana, usishangae sasa hata kuiba hajaiba. Kuna siku tulikuwa tunasafiri kwenye daladala toka ubungo kwenda posta. Humo ndani alipanda kibaka, akachomoa simu ya mtu, mwenye simu alipogundua akatangaza kwamba ameibiwa. Kibaka alipoona inataka kuwa soo akaamua kuidumbukiza ile simu kwenye begi ya mdada mmoja humo kwenye daladala.
Aliyeibiwa simu akaanzisha msako kwa kila abiria, yule mdada wa watu bila hili wala lile akalitoa begi lake kwa kujiamini kabisa lisachiwe. On her suprise simu ilikuwa mle, alikula kibao hadi anajikojolea kama si abiria wengine kuamua kumtetea. Nadhani yule dada angeishia pale. Yule kibaka baada ya kuona abiria wameanza kuweka doubt alitoka mbio za ajabu. Hata kumkimbiza ilikuwa vigumu.
Kila siku huwa nakumbuka ile incidence halafu najiuliza, kwamba suppose ile simu ingetumbukizwa kwenye mfuko wa suruali wa kijana mmoja mchafuchafu aliyechoka na maisha? Au suppose abiria wasingejenga moyo wa kumwamini yule dada wakaamua kumkomalia kwa mawe na manondo?
Kwakweli kuwe na mipaka katika maamuzi ya kumpiga mtu kwa kumhisi kuwa ni kibaka.
Kuna incidence nyingine ilitokea mabibo hosteli waliowahi kuishi huko wanaweza kuwa wanaifahamu. Mkaka wa watu akauawa kwa kudhaniwa ni mwizi kumbe ni ugomvi kati yake na girlfriend wake. Tuwaelimishe wananchi juu ya hatua hizi za kujichukulia sheria mikononi.