Hivi neno baka(T) linahusiana kibaka?na kama ndio mtu akibakwa anaweza sema amebakwa na kibaka?na mtu akiporwa kitu na kibaka atakuwa amebakwa na kibaka.?na yule mbakaji kwa nini hatumuiti kibaka!..
MSAADA KWENYE TUTA
Hapana, hayo maneno hayahusiani kwani yana maana mbili tofauti kabisa.
Neno 'baka' lina maana mbili.
Linaweza kumaanisha alama au doa juu ya mwili. Kwa mfano, mtu mwenye mabaka mabaka usoni na/au mgongoni - utango utango. Hapa, hilo neno limetumika kama nomino.
Lakini pia, hilo neno linaweza kutumika kama kitenzi elekezi na kumaanisha kumkamata mtu kwa nguvu aghalabu bila ridhaa yake na kuzini naye; najisi.
Kibaka, (nomino) ni mtu mwenye tabia ya kupora vitu aghalabu kwa watu wapitao njiani.
Hivyo, unabakwa na mbakaji na unaporwa na kibaka.
Kwa Kizungu, mbakaji=rapist; kibaka=pickpocket.
Ila, kwa kutegemea na muktadha neno mbakaji laweza kutumika kumaanisha mporaji pia.