"Mtia nia wa mtaa wa Mji Mpya uliyopo kata ya Kwembe Jimbo la Kibamba amekatwa kwa sababu tu aliandika kazi ni mjasiriamali, hivi kwani jamani ujasiriamali siyo kazi? Kwenye mtaa huu ameteuliwa mjumbe 1 tu ambae aliandika kazi ni dereva." - Rahma Mwita kupitia ukurasa wake wa X
Kuna ujinga mwingi mno kwa wagombea wote na wa vyama vyote na wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi huu kwa sababu hawazijui sheria na kanuni za uchaguzi huu..
Inashangaza sana tunapokuwa na msimamizi msaidizi amepewa dhamana ya kusimamia zoezi nyeti kama hili la uchaguzi lakini anakuwa hajui sheria na kanuni zinazoongoza na kusimamia mchakato mzima wa uchaguzi...
Na hapa inawezekana wakawa hawajui kweli (wajinga) au ni mkakati wao wa makusudi wa kutumia ujinga wa kutojua wa baadhi wa wagombea hususani wa vyama vya upinzani kuwanyima haki zao za kisiasa kama hii ya kuchaguliwa kuwa viongozi...
Vyama vya siasa ni lazima vitoe elimu kwa wanachama wao na wahakikishe wanaijua sheria na kanuni zinazosimamia mchakato wa zoezi la uchaguzi huu...
Vyama msiitegemee serikali hii chini ya CCM ambao nao wana maslahi ktk uchaguzi huu watoe elimu kwa wapiga kura na wagombea..
Hii ni kazi yenu. Hii ni vita na ni lazima mpigane na kushinda. Acheni kulala na kulalamika tu...?
==============================================
UTARATIBU WA MAPINGAMIZI UKO VIPI?
1.
KWANZA; Muda wenyewe wa mapingamizi na kisha mgombea kuwa disqualified bado haujafika kwa mujibu wa kanuni ya 23. Sasa hili limetoka wapi? Bila shaka ni hii ni psychological frustration tu kwa wapinzani ili wakate tamaa na kurudisha majeshi nyuma ikibidi wakimbie kabisa...
2.
PILI; Wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi (ambao ni watendaji wa vijiji/mitaa) katika localities zao, kazi yao kisheria ni
kutoa na
kupokea fomu za uteuzi zote toka kwa wagombea wote...
3.
TATU; Kwa mujibu wa sheria na kanuni hiyo hiyo ya 23, "
siku ya uteuzi wa wagombea" ni kesho
J'mosi tarehe 8 kuanzia saa 2:00 asb - 10:00 jioni
NB:
Kumbukeni maana ya "Siku ya uteuzi wa wagombea" kwa mujibu wa sheria ni siku ambayo MSIMAMIZI WA UCHAGUZI (ambaye ni Mtendaji wa kijiji au mtaa) kuanzia kati ya saa 2:00asb - 10:00 anatakiwa na sheria kubandika majina ya wagombea wote wa vyama vyote vya siasa katika mbao za matangazo za ofisi ya kijiji/mtaa bila kujali fomu hizi zimeandikwa nini au zina makosa gani au zimekosewa kitu gani...
4.
NNE; Baada ya majina ya wagombea wote toka vyama vyote vya siasa kuwa yamebandikwa kwenye mbao za matangazo za ofisi za kijiji/mtaa, basi ndani ya siku mbili (tarehe 9 & 10/10/2024) huo ndiyo muda wa wagombea wenyewe kuchunguzana na kisha kuwekeana mapingamizi kama yapo...
5.
TANO: Msimamizi msaidizi wa uchaguzi (mtendaji wa kijiji au mtaa) atapaswa ndani ya siku hizo mbili (tarehe 9 & 10 mwezi huu wa 10) kupokea mapingamizi yote yaliyowasilishwa kwake kwa maandishi..
6.
SITA; Msimamizi msaidizi wa uchaguzi kwa mujibu wa sheria na kanuni anapaswa kuyatolea maamuzi mapingamizi hayo ndani ya siku mbili baada ya siku ya mwisho ya kuweka mapingamizi kuisha ambayo ni tarehe 10/10/2024. Siku za kusikiliza na kutolea maamuzi mapingamizi ni tarehe 11 & 12/10/2024..
7.
SABA; Wanaoruhusiwa na sheria kuweka mapingamizi ni:
(A) Wagombea na
(B) Walioomba uteuzi na (labda) fomu zao kukataliwa kupokelewa na msimamizi masaidizi wa uchaguzi kwa sababu anazojua yeye
NB:
Wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi (Watendaji wa vijiji/Mtaa) au mtu mwingine yeyote nje ya hao ☝🏻☝🏻 wanaotambuliwa na sheria hawana mamlaka kumwekea pingamizi mgombea yeyote. Kama kuanzia kesho kutwa kutakuwa pingamizi la namna hii, basi hilo pingamizi ni batili na haramu, ni la kijinga kutoka kwa mtu mjinga lisilostahili kusikilizwa hata kwa dakika moja tu...!
8:
NANE; Sababu ambazo zinaweza kumwondolea sifa mgombea yeyote kuwa mgombea wa uongozi zimetajwa katika kanuni za 15 na 16. Katika zote, hiyo ya inayotajwa kwenye fomu hiyo uliyoiambatanisha haipo. Kwa hiyo hata kama kuna pingamizi litatolewa kwa kutumia sababu hiyo, pingamizi hilo ni batili na halimwondolei mgombea sifa ya kuwa mgombea kwa mujibu wa kanuni ya 15 na 16 zikisomwa kwa pamoja...