Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
Baada ya Rais Samia Hassan Suluhu kuwa mgeni rasmi wa kikao kazi cha Maafisa Habari wa Serikali kinachofanyika kwenye Ukumbi wa Mlimani City, jana Jumanne Juni 18, 2024, Kongamano linaendelea Jumatano Juni 19, 2024.
KIBANDA: KAMPUNI YA MAGAZETI YA SERIKALI (TSN) INA HALI NGUMU, ISINGEKUWA YA SERIKALI INGEFUNGWA
Mwanahabari Mkongwe Nchini, Absalom Kibanda amesema Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari alikengeuka alipounda Kamati ya Kutathmini Hali ya Vyombo vya Habari iliyokuwa chini ya Mwenyekiti, Tido Mhando.
Amesema Kamati hiyo haikuwa na uwakilishi wa Serikali ambaye ndiye Muajiri Mkuu wa Vyombo vya Habari kwa kuwa Vyombo vinavyomilikiwa na Serikali pia vina hali mbaya kiuchumi, akitoa mfano Waandishi wa Habari wa Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN) nao wana hali mbaya kiuchumi.
Ameongeza "Leo hii Wafanyakazi wa TSN wameshindwa kujiendesha, mishahara yao imeenda kutolewa Hazina, hivyo kama kusingekuwa na nguvu ya Serikali ingekuwa imeshafungwa."
Pia Soma
~ Kuna dalili ya upigaji wa Fedha za SACCOS za Wafanyakazi wa Magazeti ya Serikali (TSN), Waziri Nape tusaidie
~ Mazingira ya kazi kwa Vibarua wa Magazeti ya Serikali si mazuri, mamlaka ziangalie malipo wanayopata
KIBANDA: VYOMBO VYA HABARI NI TAASISI ZA KIUSALAMA WA NCHI
Mwanahabari Mkongwe Nchini, Absalom Kibanda amesema "kufa" kwa Vyombo vya Habari ni tishio kwa usalama wa Nchi na sio suala la ajira tu, akiitaka Serikali kuwa na mpango mkakati hata kama ni wa kimyakimya kusaidia tasnia hiyo.
Kibanda ameyasema hayo katika Kongamano la Maendeleo ya Sekta ya Habari kwenye Ukumbi wa Mlimani City, Dar es Salaam, leo Jumatano Juni 19, 2024.
KIBANDA: HALI NGUMU YA VYOMBO VYA HABARI, IMEZALISHA KINA MANGE KIMAMBI KWA KUWA KUNA OMBWE
Akichangia mada katika Kongamano la Maendeleo ya Sekta ya Habari, Mwanahabari Mkongwe Nchini, Absalom Kibanda amesema hali nguvu ya kiuchumi imesababisha kuwe na nafasi kubwa ya baadhi ya Watu wasio kuwa na tasnia ya Habari kuingilia taaluma hiyo.
Amesema kama hatua hazitachukuliwa kuokoa Tasnia ya Habari kuna uwezekano mkubwa wa kuendelea kuzalisha Watu wa aina hiyo kwa kuwa kuna ombwe.
SALOME: BAADHI YA MAMBO YANACHANGIA UOGA WA KURIPOTI HABARI ZA UCHUNGUZI
Mwandishi Mwandamizi Salome Kitomari anasema baadhi ya mambo ambayo yamekuwa yanakwaza maendeleo ya Sekta ya Habari na wakati mwingine kuchangia kuwa na uoga wa kuripoti Habari za Uchunguzi.
Ametoa mfano suala la Sheria ya umiliki wa Vyombo vya Habari inayomwelekeza Mwekezaji kutoka nje kuwa na ukomo wa umiliki wa Asilimia 49 wa hisa kwenye uwekezaji, anasema hiyo inazuia wale wanaotaka kufanya mambo mkubwa.
Anasema “Kamati iliyoundwa na Waziri kutathmini Hali ya Vyombo vya Habari yenyewe imependekeza kuondolewa kwa Sheria huyo kwa kuwa imeona haifai.
“Lingine ni ulipaji wa Leseni Tsh. Milioni moja kila Mwaka, unakwaza kwa kuwa kuna wakati inaweza kutumika kama fimbo, mbona wawekezaji wa simu wanapewa leseni ya Miaka 25 kwanini isiwe kwenye Habari!”
Aidha, amesema Sheria ya Epoka imetengeneza mazingira ya kutozitambua au kuzidogosha Redio za Kijamii, badala yake zinatakiwa kutambulika kuwa Redio za Kibiashara, hivyo ametoa wito kuwa Redio hizo zinatakiwa kutengenezewa mazingira ya kulipa kodi na tozo.
USALAMA WA WAANDISHI WA HABARI
Msemaji wa Jeshi la Polisi, David Misime anaelezea: Jukumu letu ni kulinda mali za Watu na mali zao, wakiwemo Waandishi wa Habari, pamoja na hivyo muhimu ni kufuata Sheria zinazoelekeza.
Kuna miongozo na Kanuni juu ya kufanya nao kazi hata kama kuna mazingira ya hali ya usalama sio mazuri, pia tumekuwa tukiwapa maelekezo na mafunzo jinsi ya kufanya kazi katika mazingira tofauti.
Tunafanya makongamano na mijadala na Waandishi wa Habari, juu ya kufanya kazi pamoja, kuelezana mipaka ya pande zote mbili.
Hivi juzi mlisikia Rais aliunda Tume ya Haki Jinai na mojawapo ya yaliyojadiliwa ni jinsi ya Jeshi la Polisi kufanya kazi na Jamii.
Kutenganisha uhalifu na kuvuja taarifa binafsi
Sheria ya Usalama wa Taifa ya Mwaka 1970, inasema taarifa ambayo ni ya siri ambayo hautakwi kupita kwenye mifumo mingine ni kosa, ikitokea Mtu ameipata akaisambaza ni kosa.
Sheria ya Mitandao pia ukisambaza taarifa ambazo zipo kwenye uchunguzi, Mtu nashindwa kukwepa, anaingia kama ilivyo, sijui anatafuta followers.
Polisi tuna mchakato wa kupunguza sana uvujishaji wa taarifa, siku zijazo tutaona matokeo ya huo mchakato.
Haki ya Dhamana
Kuhusu Dhamana, zipo za Polisi zipo za Mahakama, Sheria inaeleza Mtu gani anatakiwa kupewa dhamana na katika mazingira gani na ni Mtu gani anatakiwa kupewa dhamana.
Mfano Uchunguzi wangu wa awali ukinionesha kwamba kupitia wewe naweza kufika sehemu fulani, lazima nitaendelea kuwa na wewe, tatizo Watu tunaenda kwenye Haki bila kuangalia mazingira ya uhalisia.