Kibatala: Nani alimuua Akwilina? Iundwe tume

Kibatala: Nani alimuua Akwilina? Iundwe tume

Shujaa Mwendazake

JF-Expert Member
Joined
Jul 11, 2015
Posts
4,016
Reaction score
6,759
"Sasa hivi hukumu imewaachia huru akina Mbowe wito wangu kwa wale wote wenye Mamlaka ambao wanalifuatilia suala hili wafanye juhudi waweze kuwaambia wananchi ukweli nini hasa kilitokea kuhusu yule binti (Marehemu Akwilina)"

- Wakili Peter Kibatala
 
Kuwajibika kwa matendo mabaya ya polisi ni tendo la kiungwana.
 
Kwanini tupoteze mda na pesa kwenye tume wakati mtuhumiwa mkuu ni yule Boss wa mkoa na wanausalama wengine kipindi kile.
 
Yaani mateso ya watanzania wenzetu hawa pamoja na familia zao ni makubwa mno,unyama huu ni zaidi ya unyama wa kikaburu kule Africa ya kusini,ipo siku haki kwa watu hawa itapatikana.
Binadamu ni katili sana.

Unamuua mtu hajakukosea lolote!

Huwezi amini kama aliyefanya haya ni Mtanzania mwenzetu.
 
Kwanini tupoteze mda na pesa kwenye tume wakati mtuhumiwa mkuu ni yule Boss wa mkoa na wanausalama wengine kipindi kile.
Ndio Tunataka Tume iwataje ili tuwapeleke Mahakamani Suala la Kupoteza Hela usijali Kuna Wabunge fake 19 Walipwa Mil.11 kila mmoja kila Mwezi Tanzania TAJIRI SANA
 
Ni lazima, vyovyote iwavyo, kama si leo au kesho, wauaji wa Akwilina na wengineo, hata kama wakati huo watakuwa vikongwe, wasimame kizimbani. Na wale wote wenye mamlaka ambao walizuoa haki kutendeka, nao lazima wahukumiwe.
 
Back
Top Bottom