mtokeibwima
Member
- Aug 2, 2014
- 72
- 36
Yaani TANESCO KIBITI mnatia aibu sana. Kila siku umeme hauwaki mfululizo zaidi ya saa moja au mawili. Hii haijalishi ni usiku au mchana. Yaani ni mwendo wa washa zima. Mjitafakari sana.
Na msivyo na aibu mnasema eti ni miundombinu wakati tangu umeme umeingia wilaya ile haijafika miaka 10. Ni uchakavu gani huo wa kiboya boya.
Mjitafakari kwenye utoaji huduma wenu hapa Kibiti. Shame on you

TAARIFA KWA WATEJA
Tunasikitika kuwataarifu wateja wetu kwamba tumepata changamoto ya kudondoka kwa nguzo nane eneo la mbande chamazi hivyo kusababisha laini ya Somanga kukosa huduma ya umeme kwa baadhi ya maeneo.
MAENEO YANAYOKOSA HUDUMA YA UMEME
Baadhi ya maeneo ya wilaya ya mkuranga
Wilaya ya Kibiti yote
Wilaya ya Rufiji yote
JITIHADA ZINAZOENDELEA
Wataalamu wetu wapo site kuweza kutatua changamoto hiyo, wanasimamisha nguzo eneo la chamazi.
MUDA WA KURUDI
Kutokana na ukubwa wa kazi tunategemea huduma ya umeme itarejea saa 7 usiku
Shirika linaomba radhi kwa usumbufu unaojitokeza
Imetolewa na Ofisi ya
Uhusiano na Huduma kwa Wateja
**TANESCO PWANI
28/04/2024**View attachment 2976242