Habari za asubuhi madoctor wa JF, mm nina tatizo limenianza siku ya tatu sasa, kibofu kinawaka moto, mkojo unanibana kila mara na nikienda kukojoa mkojo unatoka kidogo ukiambatana na maumivu makali sana. Watu wamenishauri ninywe maji na matango lakini tatizo liko palepale. Naombeni ushauri wenu kwa mnaofahamu hili ni tatizo gani na tiba yake mnisaidie nipate kupona.
Unasumbuliwa na UTI(URINARY TRACT INFECTION)hizo ndio dalili zake.Kwahio ni lazima uende kwa daktari ili achukue culture ya mkojo wako.UTI ni ugonjwa wa kawaida kwa wanawake walio sexualactive kwasababu viungo vya uzazi vya mwanamke vipo karibu na kibofu.
Na akupatie antibiotics,chaguo la kwanza ni
triometaprim-sulfamethazole,chaguo la pili ni
nitrofuranotin
na la tatu
pevicillinam.Zinaweza kutumika pia amoxicillin(beta lactams)ila kuna tatizo la resistence.Ni muhimu kumaliza antibiotika cure yote ili kuviua hivo vijidudu vyote vinavyosababisha hio infection au utapata tena infection na ikitokea hivo ndivo inavyokuwa ngumu kutibu huo ugonjwa kwasababu unaongeza possibilities za resistence
RESISTENCE:Is when bacteria develop mechanisms of defence to survive from the antibiotics.
Ili kuepuka kupata tena UTI:
1.Kunywa maji ya kutosha
2.Ukikojoa hakikisha unakojoa mkojo wote uliopo kwenye kibofu coz mabaki ya mikojo ndo yanasababisha vijidudu na hatimae infection.
3.Kojoa dakika 15 baada ya kujamiiana
4.Muhimu ukienda chooni kama hunawi/unatumia toiletpaper ujifute kutoka mbele kwenda nyuma na sio vice versa kwasababu kwenye sehemu ya haja kubwa kumetawaliwa na bacteria anayeitwa
E coli huyu akija kwenye sehemu ya haja ndogo husababisha infection
5.Kunywa cranberry juice kama inapatikana inasaidia sana kutibu UTI kwasababu inasafisha kibofu
6.Kapime magonjwa ya zinaa kama kaswende na kisonono