mwakani naolewa

Senior Member
Joined
Jul 25, 2024
Posts
148
Reaction score
426
Nabii kiboko ya wachawi aingia mtegoni na kuthibitika kua kweli ni tapeli baada ya Mwandishi kutoka Mwananchi Digital kupiga simu kwa kiboko ya wachawi na kujifanya mgonjwa na kiboko ya wachawi aliomba shilingi milioni kumi ili amponye.

Licha ya Serikali kulifungia Kanisa la Christian Life (CLC), lililoongozwa na Dominique Dibwe maarufu kama ‘Kiboko ya Wachawi’, imebainika kiongozi huyo wa dini anaendelea kutoa huduma hiyo, huku akiomba mamilioni ya fedha kwa waumini wake.

Tofauti na awali, Dibwe ambaye ni raia wa Jamhuri ya Demokrasi ya Congo (DRC) kwa sasa anatoa huduma ya maombezi na kile anachokiita uponyaji kwa njia ya simu, akiomba kulipwa mamilioni hayo kwa waumini wenye matatizo.
Your browser is not able to display this video.
Soma pia
>Kufungiwa kwa kanisa la “Kiboko ya Wachawi” pongezi kwa Serikali
 
Ndo tabu ya kuhama hama madhehebu kama mbuzi wanavyokula kila mti...
Huyo mbaba ni mjinga sana ngoja awalie hao wanaomtumia hela eti milioni 10...lol kwamba yy ndo mleta uhai au?.
Nadhani wale wahangaikaji wamesikia hapo
 
Tatizo ujinga upo Kwa wtz wengi sana.Na amini huyu kiboko ya wachawi angekuwa kwenye Nchi ambazo raia wake wanajitambua kama Canada au china asingepata hao wateja mbulula wa kulipa fedha nyingi ili waombewe.
 
Hii Dini ni ya kitapeli sana ila aha waibiwe tu maana wanajidai wamesoma sana kuna hawajaeleimika kabisa
MASHETANI WAMEIINGILIA DINI YA KIKRISTO NA WANATAKA KUIANGUSHA, NI BUDI WAKRISTO KUSIMAMA IMARA KUISIMAMIA DINI HII, SHETANI APOKONYWE DINI YETU, IRUDISHWE KWENYE MSINGI YAKE MIKUU, THANKS SO MUCH MASAUNI ZIDI KUFUNGIA MATAPELI HAYA, MAJIZI!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…