Mimi ni miongoni mwa watu wanaozichukia sana hizi huduma za watu binafsi za kidini. Kama kweli wana hizo nguvu za kuleta utajiri, kuondoa magonjwa n.k basi wote wakusanywe uwanja taifa waombee watanzania wote wawe matajiri na wapone magonjwa yanayowasumbua.
Suguye anakusanya kucha na nywele za utosini akidai anaziombea ili mtu akombolewe kiroho.
Mzee wa upako yeye anakusanya fedha kutoka kwa waumini kwa minajili ya kuwaombea (hao waumini) wapate utajiri.
Mwamposa amechimba kisima cha maji halafu anawauzia waumini maji hayo ambayo si salama, kwa madai kuwa yatawaponya.
Dr. Sule yeye anahubiri kuwa uislam na majini ni damu damu. Na anasema ukiwa ni muislam halafu aukayachukia majini basi wewe siyo muislam.
Wapo akina Masanja Mkandamizaji, Luka Tony, Sophia n.k ambao makanisa yao ni kama majukwaa ya unyago kwa namna yalovyojikita kuhubiri masuala ya mahusiano.
Swali: Huyu kiboko ya wachawi kafanya jambo gani ambalo serikali inaliona ni la ajabu sana kuliko hayo niliyoyaeleza hapo juu? Na je, serikali imeridhia utapeli wa hao wengine kuendelea kufanyika kwa watanzania?
Nimalizie kwa kusema kuiga siyo vibaya. Tuige kwa rais wa Rwanda aliyewafutia vibali watu 600 waliokuwa wakiendesha huduma za kiroho, na kisha kuweka vigezo vigumu kwa mtu kuanzisha kanisa binafsi.
Kama serikali iko serious iyafute makanisa binafsi yote, halafu tuanze upya. Kila anayetaka kuanzisha atoe maelezo ya kina kwann hataki kuchangamana na main churches.
Ni hayo tu.