GE2025 Kibonde: Nikiwa rais nitagawa Bodaboda kwa kila kijana

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

DuaZaMama

JF-Expert Member
Joined
Jun 2, 2025
Posts
1,882
Reaction score
4,153
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama cha Makini Costa Kibonde ametoa ahadi ya kugawa boda boda Milioni moja na kuzigawa bure kabisa, lakini lazima wanufaika wapate cheti cha mafunzo endapo atachaguliwa kuwa Rais.

Ndugu Kibonde ameyasema hayo wakati akinadi sera zake katika Jimbo la Mbeya Mjini ambapo amesema, "Vijana wengi nchi nzima wanajihusisha na Boda boda na tumebaini ya kwamba, boda boda hizo ni za mikataba. Hivyo basi, serikali ya Chama cha Makini inakwenda kutoa boda boda milioni moja na kuzigawa kwa vijana bure kabisa. Vijana mkae mkao wa kupata bodaboda bure" Alisema Kibonde.

Aidha Mgombea huyo amesema masharti ya kupata bodaboda hizo ni lazima vijana hao wapate mafunzo maalumu na cheti, "Ila masharti yake ni kwamba lazima muende kozi ndogo na mpate cheti na hatimaye kwa kuwa mimi tarehe 05 mwezi wa kumi na moja baada ya kula kiapo cha Urais, nikiingia Ikulu nitatoa amri kwa maafisa usalama barabarani wawapatie vijana wa bodaboda leseni ili wawe na sifa ya kuja kuchukua bodaboda za bure ambazo zinatokana na serikali ya Chama cha Makini" Alisema Kibonde.


Pia Soma: Chama Makini waahidi kutoa bodaboda milioni 1 kwa vijana endapo watashika dola
Your browser is not able to display this video.
 
Heading yako;
kibonde-nikiwa-rais-nitagawa-bodaboda-kwa-kila-kijana.

Mbona ni tofauti na content ?

Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama cha Makini Costa Kibonde ametoa ahadi ya kugawa boda boda Milioni moja na kuzigawa bure kabisa, lakini lazima wanufaika wapate cheti cha mafunzo endapo atachaguliwa kuwa Rais.
 
Chama kinaitwa MAKINI, ndio nini hiki? au ni DEMOKRASIA MAKINI?. Huyu mgombea hata aseme atagawa gari hakuna anayemuelewa. Kwanza chama chenyewe hakijulikani kwa wananchi atashindaje?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…