expirience man
JF-Expert Member
- Nov 16, 2013
- 214
- 104
Niseme tu kuwa sijatumwa na mtu yeyote kuleta uzi huu hapa Jamii forum ila ni utashi wangu binafsi kwa namna vile namfahamuatajwa happy just.
Kibondo Kama Jimbo muhimu la uchaguzi katika mkoa wa Kigoma na wilaya ya muda mrefu Sana , nami ninasukumwa kwa utashi wangu binafsi kuwahamasisha ndugu zangu awamu hii kutafuta mtu atakaetusaidia kutusogeza hatua muhimu za amendeleo.
Jimbo la Kibondo Mjini kwa nyakati tofauti tumepata wabunge kutoka vyama tofauti kwa nyakati tofauti lakini wote hawajakuwa msaada wa kutusogeza wanakibondo.
Maana maji, umeme kwa baadhi ya maeneo ya kando ya mji mpaka Leo imekuwa changamoto kubwa kwetu, Kama hatuna muwakilishi vile bungeni.
Ukitupia macho upande wa shule za kibondo kuanzia msingi na sekondari na ufaulu wake umekuwa uko chini Sana.
Miundombinu ya barabara Kuna vijikilomita vichache Sana hapa mjini na hata hizo barabara chache zilizochongwa ni kwa msaada wa mashirka ya wakimbizi.
Na hapa niseme tu kwa kifupi kuwa wilaya ya Kibondo Mjini bila uwepo wa mashirka ya kuhudumia wakimbizi bado ni changamoto kubwa kubwa sana.
Tulipata bahati katika baraza la mawaziri la mh JPM mbunge wetu Atashasta Nditiye alipata unaibu Waziri wa Mawasiliano, na kwa hilo tukashukuru sana tukadhani labda wakati huu tutapata maendeleo lakini hakuna kitu hata kimoja amefanya Nditiye kwa wanakibondo.
Sasa hapa nisiseme mengi sana wakati unakuja tutaweka mambo hapa kwa takwimu watu wa Kibondo wapate kuelewa nini namaanisha, lakini hapa kwa uchache tu nijikite kwa wasifu wa mtia nia kwa tiketi ya CCM bwana Fredrick Stanley.
Bwana huyu ni mzaliwa wa hapa na amesoma elimu zake za msingi hapa Kibondo na baadae Tabora kwa sekondari na Advance na baadae kujiunga na chuo kikuu Cha Dar es salaam katika fani ya sayansi ya siasa.
Alifanya kazi katika mashirika ya kuhudumia wakimbizi ikiwemo kamati ya uokozi ya kimataifa (IRC) na plan international.
Mtu huyu ana maono makubwa Sana kuhusu Kibondo na Jamii ya wanakibondo.
Ni kijana asiye na kashfa yoyote ndani na nje ya chama.
Ni muadilifu asiye na mawaa kabisa.
Haya machache tutawambia wanakibondo wake kwa waume mtuletee huyu kwa muelekeo sahihi wa mustakabali wa Jimbo la Kibondo Mjini.