Kibonzo cha Kipanya leo ni kigumu kuelewa

Kirahisi tu.. Kwamba wakati wamachinga wanaanza kufanya biashara zao barabarani, waliachwa sasa wamezowea itakuwa kazi kuwaondoa
Wamachinga waliachwa wafanye biashara kiholela ili kuwa turufu ya kura kwa CCM. Sasa tatizo kimeota mizizi na wanatafuta njia za mkato kulitatua.
 
Mti umeupanda mwenyewe umekuwa mkubwa unashtuka. Wamachinga waliwekwa kama mtaji wa kiasa wakati tatizo dogo wakaliacha na kupalia kabisa wenyewe kushtuka mti umezaa sasa shughuli kuukata.
 
Kila mtaa kitolewe kiwanja kwaajili ya machinga. Wa design ghorofa yenye vizimba, vyoo na ofisi za utawala. Msiwapeleke mbali.
 
Mimi naona huo mti ulipokuwa mdogo ulikuwa Ccm(kijani) sasa umekuwa ni Cdm(kaki)
 
Sio wamachinga tu,ukipita manzese serevice road hazipo zimekuwa eneo la biashara.Hii imekuwa kero sana na nilijisemea mwenyewe zamani kuwa wanaachwa lakini wataigeuza kuwa haki yao hapo baadaye.Sasa baadaye ile niliyofikiria ipo mbali imefika!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…