Kibosho na Machame

Miiku

JF-Expert Member
Joined
Oct 8, 2014
Posts
3,835
Reaction score
2,642
MGOGORO WA MACHAME NA KIBOSHO

Kwanza nipende kuwaarifu kuwa hapo Mwanzo kabla ya utawala wa Sina hapakuwepo na uhasama kati ya Mashami na Kiwoso. Watu walikuwa wanashirikiana na kuoana toka sehemu zote mbili kama mahali pengine popote, ingawa kulikuwepo mgogoro midogo.

Sina ni jina Mangi Sina alilopewa na Wamachame kwa sababu ni mtoto wa kambo aliyekulia kwenye familia ya Mangi Shangali na alikuja Machame wakati mama yake alipoolewa na Mangi. Unajua tena wakati ule Mangi alikuwa anaoa wake wengi. Sina alipewa jina hilo kwa sababu ya kupenda kula nyama zenye mifupa.

Wakati alipopelekwa kutawala sehemu ya Kiwoso, watu wa Kiwoso waliomba mtawala kutoka kwa Mwitori (Mangi Shangali) kwa sababu Mchili aliyekuwepo alikuwa amekufa. Kwa sababu ilipambana na kipindi ambacho Mangi Shangali alikuwa amegawa jimbo la Hai kwenye sehemu tano, basi Sina akatawazwa kuwa Mangi wa Kiwoso.

Alipoanza kutawala Kiwoso alikuwa anafahamu siri nyingi za Mangi wa Hai na Mashami kwa sababu ni mtoto aliyekulia kwenye familia ya Mangi. Alikuwa anawafahamu majemadari wote wa vita wa Machame. Lakini alingiwa na tamaa ya kutawala Hai yote na kama angechukua Mashami basi lengo lake lingetimia maana ndipo kulikuwepo na Mangi Shangali.

Ili kutekeleza lengo lake, Mangi Sina alijifanya kuwa amekufa na taarifa ilipelekwa kwa Mangi Shangali. Mila iliyokuwepo ni kwamba Mangi akifa anakwenda kuzikwa na majemadari. Majemadari wa Mashami waliondoka kwenda Kiwoso kwenye Msiba kushirikiana na wenzao wa Kibosho

Walipofika kwenye Ngome ya Mangi Sina walitakiwa waache silaha zao nje. Dada zao waliokuwa wameolewa Kibosho waliona huruma kwa ndugu zao watakavyoingia kwenye shida na wakawa wametoboa ndizi kwa vijiti na kutupa njiani ili watakapoona wakimbie wajue siyo msiba bali ni vita. Lakini ni majemedari wawili tu walitambua na kutoroka kupitia msituni.

Walipoingia kwenye Kasri kumbe Sina alikuwa amechinja mbuzi akamwacha aoze na alinuka wakaona wafanye kuzika haraka. Kabla ya kufanya hivyo ndipo wajemedari wote walioingia kwenye Kasri waliuawa na waliofanikiwa kutoka nje ya Kasri walijikuta wakikimbizwa kuelekea kwenye dimbwi kubwa lilikuwa kwenye mto uliokuwa karibu na Kasri. Jeshi lote la Mashami lenye nguvu za kivita na ulinzi liliishia huko. Kwa Mashami ulikuwa msiba mkubwa kwa sababu karibu kaya zote zilikumbwa na msiba (ni kama mithili ya yaliyotokea Rwanda).

Mangi Sina alijua tayari nimeshadhoofisha utawala Mashami na akataka kuja kuvamia Mashami. Lakini kwa bahati mzuri au mbaya ndipo na mkoloni akaingia na Mangi Shangali aliwapokea na ndipo wakaleta usuluhishi wa kupoozesha mgogoro huo. Mangi Sina hakuweza tena kuendelea na lengo lake.

Mgogoro huu ulileta laana ambayo imegawanya hizi sehemu mbili. Maana Wamashami waliweka uhasama kuwa:
-Wamashami wote wakijenga nyumba milango au mbengye haiwezi kuelekezwa Kiwoso.
-Wamashami walikuwa wakipita kwenye ardhi ya Kiwoso walitakiwa wabebe kibuyu. Ni afadhali wakojoe kwenye kibuyu kuliko kukojoa kwenye ardhi ya Kiwoso.
-Hakuna tena mtoto wa Mashami kuoa au kuolewa Kiwoso.

Hapo nyuma miaka ya 1960-1980 kulikuwepo na msemo kuwa Dimbwi walipofia Majemedari wa Mashami lilikuwa linachemka na kutoa sauti na lilikuwa linawaletea shida zile familia zilizoshiriki kwenye mauaji. Ili kulituliza watoto walikuwa wanakuja kuibiwa Mashami na kutumbukizwa kwenye hilo Dimbwi . Hatujui kama hayo mpaka wakati huu yapo

Ninatoa rai kwa Wakuu wa Dini na Kiroho (Wachungaji, Maaskofu, Manabii na wengine wanaofanana na hao). Kukutanisha wawakilishi au wakaaji kutoka Kiwoso na Mashami ili kufanya maombi maalumu (special prayer) kuomba kwa Damu ipitayo Damu zote (Damu ya Yesu) ili kuondoa hii laana ambayo imekwenda kwenye vizazi vingi, ili watu wa sehemu hizi mbili wafunguliwe na wawekwe huru. Neno la Mungu linasema yote yanawezekana kwa yeye aaminiye.

Picha inayooneka chini ni ya kuchora ya MANGI SINA
 
Hiki ni kitabu kinachozungumzia habari za wachaga wote wanaojulikana..... Sina uhakika Kama kinapatikana tena kokote maana aliyenipa ni author mwenyewe na miaka mingi imepita. Natamani mleta mada ukipate kikuongeze uelewa kuhusu hao wakyoso na wamashami....
 
Kwa hivyo huyu Mushi Mangi sina ambaye jengo lake lipo sehemu inayoitwa kwa "Mangi " ambaye alikuwa ni mnyanyasaji mkubwa wa maskini na watu walioonekana kuwa wajuaji au wenye nguvu za kivita akikuwa ni MMACHAME?
 
Aika meku wana
 
Aisee... Nakumbuka story ya babu yetu mkubwa. Alikuwa askari ktk jeshi la mangi sina. Kipindi hicho mangi ni kama mfalme ktk eneo analitawala. Huvyo huwa anachukua baadhi ya mifugo kwa ajili yq shughuri zake binafsi au za jumuia. Siku hiyo alitaka mifugo kwa ajili yake binafsi. Babu akapinga. Taarifa ilipomfikia mangi sina akaagiza babu akamatwe. Hapo babu alikimbizwa duh.....hauijawai kutokea . anyway, hicho kitabu ningependa nikipate. Kama ikiwzkana piga picha weka humu.
 
Mkuu chakufanya chukuwa hicho kitabu ukipeleke maktaba ata nakala moja au tafuta mtu wa stationary umpe Pakipige copy alafu ww Uwe unawaagizia watu wakakinunue
 
Wazo zuri mkuu, japo nahofia hatimiliki ya mwandishi.... Sijui Kama ataniacha salama. Ninaamini kabisa kuwa kwa Wakati ananipa hiki kitabu hakujua Kama ananipa lulu..... Kwa sasa ni cha thamani kubwa kwa sababu wapo watu Wengi na wa muhimu wanakihitaji sana. Kwa hapa wataohitaji copy waje PM, hakuna la ziada.

NB: sijatoa hata copy moja.
Mkuu chakufanya chukuwa hicho kitabu ukipeleke maktaba ata nakala moja au tafuta mtu wa stationary umpe Pakipige copy alafu ww Uwe unawaagizia watu wakakinunue
,
 
kweli Mkuu sikufikiria suala la mwandishi wa kitabu
 
Hii ni stori ya kijiweni iliyoenezwa/sambazwa na mkenya mmoja aliyeitwa Mohamed Bin Uweki Shoo miaka ya 1930s akidai yeye ni mtoto wa mangi wa huko Machame aliuzwa utumwani na Mangi Sina baada ya vita kuu ya uchaggani(1850s)

Aliuzwa akiwa mtoto mdogo huko Mombasa na akafanikiwa kukutana na ndugu zake baadae kurudi Machame na kupewa kiamba chake huko maeneo ya Lyamungo

Hii ni story ambayo watu wengi wamekuwa wakiisikia au kusimuliana mitaa ya Hai huko, haina references wala citation ni pure fiction, stories za kujipa moyo/ kama justification ya loss walioipata kwa nchi yenye karibu nusu ya population yao

****************************
Matukio hujayapanga sawa hapo Mangi Sina alipoishinda Machame alimsimika Shangali kuwa Mangi wa Machame(Shangali akiwa bado kijana mdogo) hadi leo hii Shangali ni moja ya watawala bora kabisa kuwahi kutokea Machame

Ngamini mtoto mkubwa wa Ngusero ndio alikuwa anagombea kuwa Mangi wa huko Machame kinyume na shauri aloacha Mangi Ngusero baba yao na hiki ndio chanzo au uhasama ulipoanzia baina ya pande hizi mbili watu wengi hujichanganya na kusema eti hakukuwa na chanzo cha ugomvi bali ni wivu tu, haha jamaa tuwe tunajaribu ku reason mambo,

*****************************
Stori za kwetu tunaambiwa Ngusero aliacha wosia kwa rafiki yake Mangi Sina kwamba mwanae mdogo ambae ni Shangali ndio apewe umangi badala yake huyu Ngamini akajaribu kucheza karata chafu akapindua nchi akajipa umangi kinyume hata na maelekezo ya wazee wa huko machame

Hapo ndio Mangi Sina hakuwa na changuzi nyingine zaidi ya vita dhidi ya Ngamini na watu wote walio loyal kwa Ngamini,

Bibi yangu ananiambia wanawake kutoka huko machame walipanga mstari mmoja mrefu kutokea huko nchini kwao hadi Kioso wakiimba nyimbo za kuomba msamaha huku wakiwa wamebema majani ya masale na vitu vingine vya thamani (mbuzi, ngome, watoto) kama sadaka/zawadi hii ilikuwa ni ishara ya toba (nikipata muda ntaandika hzo nyimbo na tafsiri zao)

Basi Mangi akaamua kusimamisha vita na kumsimika bwana mdogo Shangali kuwa Mangi wa Machame na Machame ikawa tulivu,

Ila makamanda wa vita wa kibosho walibaki huko kuendelea kulinda amani hadi hapo Mjerumani alivyotuma ultimatum kuwa makomando wa kibosho waondoke machame au iwe vita kitu ambacho Mangi alikataa na ndio kilisababisha vita ya mwisho wa wakoloni dhidi ya wachaga/wakibosho kutokea

Takwimu za hii vita ya mwisho zimerekodiwa vizuri kuliko vita nyingine zote katika kumbukumbu za mjerumani tanganyika

Mangi hakufa vitani, mangi hakunyongwa na wajerumani, mangi kichwa chake hakukukatwa na kupelekwa ujerumani, mangi hakuwekewa sumu kama inavyodaiwa na wengi, mangi alikufa peacefully huko nyumbani kwake tella kwa uzee

Source; Kathleen Stahl, History of Chagga people of Kilimanjaro
 
Kumbe ndio maana walinikataza kumuoa Mickness black beuty wa kikibosho. Walikuwa wakali kweli Baba, mama na wajomba zangu wa kimashami.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…