Kibu Denis arejea na kusafiri na Kikosi cha Simba SC kuwafuata Singida Black Stars

Kibu Denis arejea na kusafiri na Kikosi cha Simba SC kuwafuata Singida Black Stars

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
2,060
Reaction score
5,648
Kibu Denis ni miongoni mwa wachezaji walioungana na kikosi cha timu yao jioni hii kuelekea Singida kwa ajili ya mchezo wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Singida Black Stars.
IMG_2038.jpeg

Kibu alikosa michezo miwili ya awali dhidi ya Kagera Sugar na JKT Tanzania kufuatia safari ya kushughulikia matatizo ya kifamilia huko Marekani.

Pia, Soma: Mechi ya Simba SC na Singida Big Stars yapangiwa tarehe, huku na Tabora United kupangiwa siku
IMG_2040.jpeg

Kocha wa timu hiyo, Fadlu Davids, amesema kurejea kwa Kibu ni habari njema kwa kikosi chao. "Nina furaha Kibu Denis amerejea. Kila mchezaji yupo tayari kwa ajili ya mechi, hivyo nitachagua wachezaji bora kwa mechi dhidi ya Singida Black Stars. Tuna furaha kuwa na wachezaji wetu wote"
IMG_2041.jpeg

Mechi hiyo inatarajiwa kuwa muhimu kwa timu zote mbili, huku Kibu Denis akionekana kuwa chachu ya kuongeza nguvu kwenye safu ya ushambuliaji ya Mnyama ambaye anaongoza katika msimamo wa Ligi ya NBC kwa alama 37.

Mchezo wa Simba SC dhidi ya Singida Big Stars, ambao awali haukuwa na tarehe maalum, sasa umepangwa kuchezwa tarehe 28 Desemba 2024 kwenye Uwanja wa Liti, mkoani Singida.

Soma, Pia: Tafadhalini viongozi wa Simba Kibu Dennis arudi haraka sana kuokoa jahazi, Singida anatengenezewa mazingira ya kushika nafasi ya pili juu ya Yanga
 
Ikifungwa Singida ni kama imefungwa uto. Wataanza mwaka 2025 kwa masikitiko na masononeko
Swala la kuwashusha huko mliko tuachieni sisi tutafanya hiyo kazi. Msiwasingizie singida wala tabora
 
Back
Top Bottom