Kibu Denis kiwango chake anafaa kucheza Tanzania ila sio Simba

busha

JF-Expert Member
Joined
Jan 21, 2019
Posts
1,712
Reaction score
2,577
Kama kichwa cha habari kinavyojieleza mchezaji wa Simba Kibu Denis hana kiwango cha kucheza Simba ni mzigo,
hana footwork nzuri.

Hana unyambulifu wa mwili (body flexbility)

Pasi zake za kutoa na kupokea zinapotea kwa wepesi sana.
 
Kwa Sasa galasa Simba ni Bocco!Anatakiwa akacheze Ndondo!
Mkuu John Boco kiwango kimeshuka lakini alisajiliwa Simba akiwa na kiwango chake bora,lakini kwa Kibu ni tofauti kasajiliwa kucheza Simba akiwa na kiwango kibovu.
 
Mkuu John Boco kiwango kimeshuka lakini alisajiliwa Simba akiwa na kiwango chake bora,lakini kwa Kibu ni tofauti kasajiliwa kucheza Simba akiwa na kiwango kibovu.
Kibu anahitaji mtu wa kumjenga kisaikolojia!Anakosa kujiamini!
 
mm shabiki Yanga ila nashangaa jamaa kuja Simba na kupata namba moja kwa moja na mpira ule ila raundi ya kwanza haiishi ataanza kusugua mbao labda abadilike
 
Kwa mechi anazopata namba nampa asilimia 2%..

Kashazoea kukimbia kimbia kukwepa risasi muda wote anataka kuyaleta na uwanjani.
 
Mkuu John Boco kiwango kimeshuka lakini alisajiliwa Simba akiwa na kiwango chake bora,lakini kwa Kibu ni tofauti kasajiliwa kucheza Simba akiwa na kiwango kibovu.
Hivi Mhilu aligusa mpira?
 
Ile game ilikuwa na pressure hatari na ndo mechi yake ya Kwanza (kubwa) Ila he is the best I can guarantee that
 
Ally Mayai alisema kibu anapocheza hajiweki position nzuri ya kupokea mipira ,anaupokea halafu anaanza kushindana nao kwa nguvu na chenga ,angekuwa anajua kujiweka position nzuri ingekuwa poa sana.
Mtu kama Drogba alikuwa anawaburuza mabeki na mpira huchukuliwi lakini kibu hajui kukwepa mabeki anakaa nao tu mda wote
 
Wakina Kibu pale Simba wako wengi sana. Ni hawa: Kagere, Boko, Mugalu na mwingine yuko kwa mkopo KMC. Hawana unyumbulifu kabisa na ball control ni zero.
 
kwenye derby nilivyo ona kibu anatoka nikajua makolo wanaenda kutufunga, kibu alitusaidia sana maana alikuwa anakimbia kimbia tuu uwanjani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…