LENGISHO
Senior Member
- Sep 15, 2017
- 169
- 265
[emoji404]Waziri wa Mambo ya ndani ya Nchi, George Simbachawene amesema kuwa serikali imempatia uraia wa Tanzania mshambuliaji wa klabu ya Simba SC, Kibu Denis kwa mujibu wa Sheria ya Uraia, Sura ya 357 (Rejeo la 2002), baada ya kupokea ombi kutoka TFF kupitia Wizara ya Sanaa, Utamaduni na Michezo.
[emoji422]Waziri Simbachawenge amesema uraia wa asili wa Kibu Denis alikuwa raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), lakini amekuwepo nchini Tanzania tangu mwaka 1998, akiwa na umri wa miaka sita, baada ya wazazi wake kukimbia machafuko ya kisiasa nchini humo.
[emoji422]Waziri Simbachawene ameongeza kuwa mchezaji huyo amekuwa na nyaraka zinazoonesha ni raia wa Tanzania, ikiwemo kitambulisho cha uraia, kwani yeye alikuwa anajijua ni Mtanzania kutokana na kuingia nchini akiwa na umri mdogo, na hana historia yoyote na nchi yake ya asili zaidi ya kukulia Tanzania.
[emoji996]Uraia wa Kibu Denis ulileta mashaka Mara Tu aliposajiliwa na Simba SC Tanzania akitokea Mbeya city ambayo ameitumikia msimu uliopita na kumaliza akiwa kinara wa kufumania nyavu wa timu hiyo.
[emoji996]Kibu tayari ameichezea Tanzania mchezo mmoja na katika mchezo huo alitoa assist kwa John
Bocco