Kibu Dennis asaidiwe kisaikolojia

Kibu Dennis asaidiwe kisaikolojia

May Day

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2018
Posts
6,311
Reaction score
9,027
Kuna ule usemi maarufu ya kwamba "Ukitaka kazi ya jeshi basi lazima ugangamale".

Hivyo kwa mchezaji yeyote wa timu ndogo anapopambana na kuonesha makali ili afanikiwe kuwashawishi timu kubwa kumpa kazi, basi ajiandae pia kwa maisha ya upande wa pili wa shilingi, ambako kuna maisha ya presha. Wakati mwingine kuna mstari laini sana kati ya mchezaji na mwanasiasa, kuna wakati utatukanwa na kuna wakati utasifiwa.

Ukimuangalia Kibu pindi inapowekwa picha ya ukaribu yaani kuona uso wake kwenye chumba cha luninga, unamuona ni mtu anayeogopa. Sijui ni kwa kiasi gani timu wanaliona hili, ingawa naamini lipo linalofanyika kumsaidia.

Nakumbuka kuna wakati golikipa Metacha alidhani eti anaweza kukabiliana na mashabiki, uamuzi wa aina hii ni wa kijinga. Kikubwa ni kwa mchezaji kukumbushwa ya kuwa anachokipitia yeye wengi walishapitia, wanapitia na wataendelea kupitia. Mchezaji yeye ajikite kwenye kilichomleta pale na kupelekea mifuko kutuna mwisho wa mwezi.

Ni isivyo tu bahati ya kwamba, tasnia ya soka inajumuisha mashabiki wavumilivu na waliokosa uvumilivu, wastaarabu na wahuni.
 
Kwani kati ya Kibu Denis vs Fiston Mayele, yupi kati yao ni mkali wa kutupia magoli? Mimi nipo kijijini huku nalima mahindi ya vuli! hivyo sina kabisa muda wa kufuatilia ligi yenu.
 
Back
Top Bottom