Kibu na Ukandaji Kimataifa

Kibu na Ukandaji Kimataifa

kinje ketile

JF-Expert Member
Joined
Dec 12, 2015
Posts
5,089
Reaction score
9,664
Kibu hajaimbwa sana kwenye ligi ya NBC..! Wachambuzi hawamuoni ama wanajifanya hawamuoni.

' Role ' anayoivaa kwenye Mechi Muhimu za Kimaamuzi za Kimataifa ndizo zinazomfanya awe 'distinct'..!

Rejea Mechi Ya Al Ahly Tripoli alivyoilainisha Mechi kwa Bao lake Maridadi La Tick taka .! Isingekuwa lile bao ngoma ingekuwa ngumu.

Wachambuzi hawakumwona hapo.! Lile bao ilitakiwa lifafanuliwe kwa muda wa miezi miwili mfululizo!

Sasa kafunga mabao mawili ya 'head' dhidi ya Cs Sfaxien Limefanya mambo Mawili yatokee.

Kwanza kukata kiu cha mtu mwenye kiu ya kufa, mtu aliyekuwa anatamani maji kwa Muda mrefu...Ni Kibu Huyo.

Pili, Mechi zilizo salia Simba haitaingia Kinyonge..itajipiga kifua mbele kwamba Wale Wenye points 6 na sisi tupo, weka niweke.! Lazima kieleweke.

Ama Kweli Ubaya Ubwela ni mwaka huu..!
 
Back
Top Bottom