Kibubu challenge: Sasa imerahisishwa kwa excel

Kyatsvapi

JF-Expert Member
Joined
May 15, 2009
Posts
317
Reaction score
196
Wanajukwaa,

Heshima mbele.

Nimekuwa nikiona mpango wa baadhi ya watu kujijengea desturi ya kuweka akiba kwa mfumo ambao unajulikana kama 'kibubu challenge'.

Baada ya kujifunza namna unavyofanya kazi, nikaona na miye nichangie kidogo katika kuendeleza tabia hii nzuri ya kujiwekea akiba kwa kutengeneza 'template' rahisi kabisa kwa kutumia MS Excel ambayo itasaidia katika kuhifadhi kumbukumbu na pia kuona maendeleo ya uwekaji akiba.

Nimetengezea mafaili mawili; moja kwa lugha ya kiingereza na lingine kwa Kiswahili ili kuwapa nafasi watu wote wanaopenda kufuata mtindo huu wa uwekaji akiba waweze kufaidika na maarifa haya.

Mpangilio wa faili:
Faili limegawanyika katika sehemu kuu 3.
  • Sehemu ya kwanza inaonyesha muhtasari wa taarifa mbalimbali ikiwa ni pamoja na sehemu ya kuchagua aina ya mfumo wa uwekaji akiba unaoupenda.
  • Sehemu ya pili inaonyesha matarajio ya fedha zitakazotakiwa kuwekwa akiba kwa kila wiki kwa muda wa mwaka mzima.
  • Sehemu ya tatu inaonyesha matarajio ya fedha za akiba kwa siku ikiwa ni pamoja na jumla ya akiba kwa kila siku kwa siku zote za mwaka. Sehemu hii pia inaonyesha kiwango cha fedha halisi ambacho kimetunzwa kama akiba.

Namna inavyofanya kazi:
1. Fungua faili na chagua lugha kati ya kiingereza na Kiswahili. Nitatumia Kiswahili katika maelezo yangu.
2. Nenda sehemu ya kwanza (Muhtasari) na chagua kiwango cha riba. Ukigonga kwenye riba utaona mshale unaoelekea chini na hapo utaweza kuchagua kiwango chochote cha riba kati ya 5% hadi 30%. Hiki ni kiwango ambacho utatakiwa kukiweka kila wiki kwa akiba ya wiki iliyotangulia.
3. Chagua kiwango cha fedha cha kuanza nacho. Ukishachagua, utaona kiasi ambacho utapata kama akiba ifikapo mwisho wa mwaka.
4. Utaona pia sehemu ya pili ikibadilika mbapo itakuonyesha kiasi cha kuweka kama akiba kila wiki.
5. Sehemu ya tatu itakuonyesha kiasi cha kuweka kama akiba kila siku na namna akiba inavyoongezeka kila siku.
6. Weka kumbukumbu ya kiasi ambacho umeweka akiba katika 'column' ya mwisho ya sehemu ya tatu. Rekodi ya kiasi unachoweka itaonekana katika muhtasari.

Kwa kuwa mwanzo wa mwaka umekwisha kupita unaweza kuanza sasa kuweka akiba kwa kufidia kipindi kilichopita ambapo unaweza ona ni kiasi gani gani ulitakiwa uwe nacho (kwa tarehe ya leo) kutegemeana na plani uliyochagua.

Faili la excel kwa kazi hii unaweza kulipakua hapa chini.
 

Attachments

Na uzuri wa hii sasa unaweza kujisajili CRDB SimAccount ukafungua kibubu chako kule na unatengeneza vibubu vinne kule tofauti ambapo unaamua uweke akiba yako hata mwaka mzima bila kuweza kutoa.

Ni rahisi sana kujisajili kwa kupiga * 150*62# unajisajili na kufurahia huduma.. huhitaji tena kuweka kibubu ndani kinaweza kuibwa ukalia na kusaga meno.. Naipenda sana hii huduma.
 
Nimeipenda hii huduma
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…