Hotuba ya raisi ilikuwa wazi, kila mtu ana masikio kusikiliza alichosema, wewe umetia maneno yako ili kujirembesha kwa mafisadi, acha kubwabwaja. Raisi wa nchi hawezi kutoa kauli kama hiyo,wafanyakazi hawabadilishi kura kwa mshahara, muungwana JK alipotoka na hiyo kauli itamtesa maishani mwake milele.
Kama watanzania wana akili sawa na ya kwako basi tumekwisha.Kwanza umesema watanzania sio waaminifu, sijui umetumia vigezo gani kufikia hiyo conclusion, nasema huko ni kuropoka, kama wewe sio muaminifu then dont generalize kuwa watanzania wote sio waaminifu.Umesema kuwa kuna rushwa/ufisadi kuanzania kata hadi ikulu, that is another plain statement ambayo huna any data kuisupport, so kwa hayo mawili nadhani unasukumwa na ushabiki zaidi kuliko akili za kawaida ambazo mungu amekupa. Na kama una macho ya kifisadi hata kama ukipewa data za kujaa chumba kizima bado hutauona ukweli. Sidhani kama data unazihitaji kabla hujafungua macho yako mengine uone ukweli, vua utando wa ghiliba za kifisadi na ushabiki wako kwa CCM na uchafu wao, jivike macho ya uwazi na utambuzi, then utaona jinsi ulivyopumbazika kwa vijisenti unavyopewa kuushabikia uongo na utumwa wa CCM. Wewe ni mtumwa, tena utumwa huu ni mbaya kuliko ule wa enzi zile, utumwa wa fikra na uchovu wa kuchambua hoja na ulegevu wa kutafakari nini hali itakuwa kwa watoto na wajukuu na wajuu za watoto wetu niutumwa mbaya kuliko ugonjwa mbaya na hatari ya malaria na ukimwi.
Kima cha chini cha 350K kinawezekana, hizo ni dola mia 250. Ni hela ndogo kaka, halafu ulivyo mvivu wa kuchambua, hukubother kuhakiki mahesabu ya JK, umebandua na kubandika kama alivyosema. Hebu nijuze, umewezaje kupata trilion 6 kwa mwaka? kama serekali ina wafanyazi 350,000? Excel yangu hapa inaonyesha kuwa kwa mwezi ukizidisha 350,000X350,000 ni 122,500,000,000. Kwa mwaka ni 1,470,000,000,000. Hizo ni trilion 1.47. Sasa kaka unataka tukupe majibu wakati maswali yako umebase kwenye wrong information, kweli tutafika?
Kama wewe ni kuwadi wa kushauri mbona hukumshauri JK atoe kauli zenye hekima.Kugoma ilikuwa ni haki ya mfanyakazi na sidhani kama kwenye mahojiano kulikuwa na swala la kumpa kura JK kama sharti la kuongezwa mshahara, aliibua soo hilo mwenyewe, wacha watu walitumie kisiasa. Hizo hotuba za kuandikiwa na JM ndizo zinamfanya JK aonekane hana maana. Na je lile la kiherehere cha wasichana kupata mimba nalo unalizungumziaje? Hakuna kiongozi wa nchi aliyekwisha sema kuwa kama vipi na kura zenu sizitaki, huo ni uchuro, kwani kama angesema haiwezekani kuwalipa fedha zote hizo kw akuwa serekali haina uwezo kungekuwa na shida gani, yaani kwa kauli yake ni kuwa siwaongezei mshahara na kura zenu sizitaki.Kwanza si raisi wa nchi mwenye mamlaka ya kuongeza mishahara, hivyo kuchaguliwa kwake na kuongezeka kwa mishahara ni vitu viwili tofauti kaka-- lol
Acha, huku ni kutapatapa kwa CCM, mara JK hakusema hivyo (Tambwe) mara wameongeza mshahara kimya kimya, mara TUCTA isiingilie swala la nani watamuunga mkono kwenye kinyanganyiro cha uraisi ni kuvunja sheria-Naibu katibu Mkuu Kazi. If this is damage control mnafanya, then guys mmechelewa sana, it was suppose kufanywa kesho yake baada ya hotuba ya JK. Kama mnaanza damage control baada ya mgombea wa chadema na TUCTA kuonyesha makucha, hiyo sio control bali mnazidi kudamage. Ningekuwa wewe, ningemshauri JK akomae na kauli yake, huo ndio ujasiri, sio kuanza kutafuta watu kama wewe kumsafisha, huo sio ukomavu hata kidogo, ni woga