vibertz
JF-Expert Member
- Mar 15, 2022
- 2,474
- 4,726
Nimejaribu kufanya tathmini juu ya uchezaji wa Simba vs uchezaji wa Yanga na aina ya wachezaji wa Yanga na Simba nimekuja kuona nguvu kubwa ya Simba katika mashambulizi itabebwa na wachezaji wawili ambao ndio wenye nguvu na upambanaji wa kiwango cha juu ambao ni Kibu Denis na Mpanzu. Hawa wachezaji ni wachezaji wanaoweza kupunguza idadi kubwa ya wachezaji na kukimbia kwa eneo kubwa la kiwanja hivyo inahitajika kulindwa na wachezaji wenye akili kubwa ya ukabaji na wenye uwepesi wa kurudi golini pindi inapopigwa counter attack. Kwenye derby iliyopita Yanga iliiruhusu sana Simba kuiingia langoni mwao katika kipindi cha kwanza.
Kwa vyovyote lazima. Simba watakuja na mkakati ule ule wa kucheza kwa kasi na kutafuta goli la kuongoza kama wachezaji wa Yanga hawatokuwa makini shughuli itaishia hapo hapo ila kama watawamudu katika eneo la ulinzi basi uwezekano wa Yanga kushinda utakuwa upande wao kwavile ina watu wengi wa kuamua mechi kuliko Simba ambayo inategemea zaidi watu wawili.
Hii mechi ni kijana kutoka Morogoro Kibwana Shomari anauwezo mkubwa wa kwenda na mtu bandi bandi. Kibu Denis huwa afurukuti kwa Kibwana Shomari hivyo hii derby ana stahili kuanza upande wa beki.