Mtanzanias
JF-Expert Member
- Jul 30, 2021
- 1,747
- 3,725
Uyu bwana mdogo ni hazina ya taifa hapo badae akiendelea kujitunza vizuri, Ujio wa beki wa kimataifa Djuma shaban wengi tulijua tunakwenda kumpoteza uyu bwana mdogo lakini alituonyesha kuwa tunakosea kwani alikuwa na uwezo wa kuangalia fursa nyingine upande was kushoto na kufanikiwa kuwaweka benchi waliosajiliwa maalum kwenye iyo nafasi, Mechi ya leo ameonyesha ni kwa nini wembamba wa relí lakini treni inapita, Kucheza na mchezaji mjanja mjanja Kama morrison na kumuweka chini ya ulinzi mkali mpaka akahama nafasi sio jambo dogo, bado akaja sakho akagonga mwamba, wakaona aitoshi akaletwa Kibu denis naye mambo yakawa magumu na wakati huo mwamba wa Lusaka alikuwa keshatolewa nje, Kwangu Mimi uyu bwana mdogo alikuwa ndo man of the match,kaifanya kazi yake ipasavyo ukizingatia amekaa nje ya uwanja mda mrefu sana