Helicobacter pylori
JF-Expert Member
- Feb 15, 2013
- 424
- 283
UGONJWA WA KICHAA CHA MBWA KWA BINADAMU.
Binadamu hupata ugonjwa huu kwa kung’atwa na mnyama Mgonjwa(Mbwa, Paka, Ng’ombe nk)
Baada ya kung’atwa Virusi huzaliana na kisha kusafiri kuelekea kwenye ubongo na kisha kuzaliana na kuenea kwenye Tezi za mate, Figo na Maini.
DALILI
Hujitokeza kuanzia mwezi 1 - 3 tangu kung’atwa na mnyama mwenye ugonjwa.
1. Homa, kuumwa kichwa, kuvimba na kuwashwa koo.
2. Kuwa muoga, kuchanganyikiwa pamoja na kuwa na tabia zisizo za kawaida.
3. Maumivu/muwashosehemu iliyoumwa.
4. Kuona vitu ambavyo havipo (maruweruwe) na kufanya ajifiche kwenye kona au akimbie.
5. Kuogopa maji (hydrophobia) kutokana na matatizo kwenye koo.
6. Mwili kupooza (kushindwa kuchezesha sehemu/viungo vya mwili) na hushindwa kula chakula.
7. Mgonjwa hushitushwa na mwanga pamoja na kelele.
8. Kupoteza fahamu na kufa.
Mara Nyingi vifo hutolea siku ya 2 -10 tangu kuonyesha dalili.
UTAMBUZI WA UGONJWA
Hatua hizi zinaweza kutoa mwanga na kusaidia kwenye utambuzi.
Historia ya kung’atwa na Mbwa ama mnyama yeyote yenye kuambatana na Dalili anazo onyesha mgonjwa.
Utambuzi kamili unafanyika kwenye maabara kwa kupeleka kichwa (ubongo) wa mnyama aliyehisiwa kuwa na ugonjwa.
KINGA.
Watu pia wanaofanya kazi katika mazingira hatarishi kama madaktari wa mifugo, wanajihusisha na mifugo, walio kwenye maabara zinazochunguza ugonjwa wa kichaa cha mbwa na wale wanaotarajia kusafiri maeneo ambako ugonjwa huu upo wanatakiwa wapewe chanjo.
Chanjo kabla ya kung’atwa (Pre-Exposure Vaccines).
Dozi ya 1: Siku ya kwanza
Dozi ya 2: Siku Ya Sabaa
Dozi ya 3: Siku 21 au 28 tangu dozi ya 1.
Lakini kwa watu wanaofanya kazi katika maeneo hatarishi wanatakiwa kuangalia mara kwa Mara kinga yao dhidi ya ugonjwa na kuchanja kwa kadri itakavyo hitajika.
UKING’ATWA NA MBWA UFANYEJE?
Mbwa au paka akimng’ata mtu lakini hana dalili yeyote, Sharti afungiwe kwenye banda kwa muda wa siku 10 NA toa taarifa kwa Daktari/Afisa Mifugo aliyeko karibu.
kama hata onyesha dalili basi anaweza kuwa hana ugonjwa. Na kama ataonyesha dalili basi mnyama huyo apumzishwe na kichwa kipelekwe kwa maabara kwa wataalamu ili uchunguzi zaidi ufanyike.
Uking’atwa na mnyama yeyote osha kidonda chako haraka vizuri kwa maji safi ya vuguvugu na sabuni.
Na kama Mnyama aliyekuuma anaonyesha dalili za kichaa cha mbwa, ni vema ukamuona daktari mapema ili aweze kukuanzishia matibabu.
Kwa mtu ambaye ameumwa na mbwa na hakuwahi kuchanjwa dhidi ya ugonjwa huu
anatakiwa apewe chanjo mara 4 (Post-exposure Vaccines).
Ya kwanza siku hiyo hiyo.
Ya Pili siku ya 3
Ya tatu siku ya 7
Ya nne siku ya 14.
Kwa mtu aliyewahi kuchanjwa dhidi ya ugonjwa apewe chanjo 2 (Post-Exposure Vaccines), Moja Siku hiyohiyo na nyingine siku ya 3 baadaye.
Wito; Kinga Madhubuti ya ugonjwa wa kichaa cha Mbwa ni Kuchanja mbwa na Paka wote wenye umri kuanzia wiki 12(miezi 3) na kuendelea.
Kudhibiti Mbwa na paka wanaoranda randa mtaani.
Kwa kubofya kiunganishi hiki, utaweza kua athari kwa binadamu.
Ugonjwa wa Kichaa cha Mbwa: Fahamu Chanjo, Dalili na namna ya kudhibiti - JamiiForums
NB: Kama Hukumbuki au Hujawapatia chanjo Mbwa au Paka wako basi wasiliana nasi (Sipy Vet centre, Kinyerezi Mbuyuni DSM, [emoji338]+255764667503, [emoji391]odhisjamach89@gmail.com)