Kichepe akutana na mwanaye akiwa na miaka 16, yeye akiwa kwenye 'wheelchair'

Kichepe akutana na mwanaye akiwa na miaka 16, yeye akiwa kwenye 'wheelchair'

Sky Eclat

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2012
Posts
57,761
Reaction score
216,011
Kichepe alizaliwa mtoto wa pekee, wazazi wake walizawadiwa shamba la mkonge na ma settlers wa Kigiriki. Waliliendeleza shamba na Kiepe alisoma Kenya tangu shule ya msingi, alikuja nyumbani likizo tu.

Kiepe akiwa darasa la 10, mama yake aligundulika na saratani ya ziwa. Matibabu yaliyowezekana yalifanyika ikiwa ni pamoja na kumpeleka India lakini alifariki ndani ya mwaka mmoja tangu ugonjwa kugundulika.

Kichepe aliendelea na shule na baba yake aliendeleza shamba. Shughuli za shamba ndizo pekee zilimsaidia baba Kichepe kupata faraja.

Baada ya kumaliza shule Kichepe alirudi nyumbani kuendeleza shamba. Wakati huo baba yake nguvu zilianza kumuishia. Kichepe alifunga ndoa takatifu na Flora. Mama yake Flora alikua housekeeper wa nyumba tangu Kichepe anazaliwa.

Flora binti mzuri, kutokana na uwezo wa mama yake alimaliza darasa la 12 na kujifunza upishi ndiyo wanaita catering. Maisha ya mwanzo ya ndoa ya Kichepe yalikua yenye furaha na amani.

Maisha yalibadilika baada ya Kichepe kuuza mkonge kwa faida kubwa. Alianza kuwa mlevi na kubadilisha wanawake. Alianza kumdharau Flora. Ugomvi ulizidi na nyumbani hakuwa anaonekana.

Siku isiyo na jina alimfukuza Flora na mabegi yake nje ya nyumba. Flora aliondoka akiwa na ujauzito mchanga pasi Kichepe kufahamu. Alikwenda kwao na kuendelea na maisha yake.

Alijufungua mtoto wa kiume, aliapa kufanya kila awezalo kumlea mtoto wake. Alianza biashara ya kuuza maandazi, alihamia mjini ili mtoto wake aweze kusoma English Medium kwani kule kijijini hakuwa na usafiri.

Alipanga chumba kimoja na aliishi na mtoto wake. Hakutaka kabisa watu wamfahamu. Baba Kichepe alifariki mapema tu baada ya Flora kufukuzwa nyumbani. Msongo wa mawazo baada ya kumuona Kichepe anatawanya mali aliyoitunza kwa miaka mingi.

Kichepe alipata ajali mbaya sana, aliuza mali nyingi kujihudumia. Siku moja akiwa anatafuta chakula akiwa kwenye wheelchair akitokea hospitali, aliona mgahawa mdogo lakini ni nadhifu sana. Kuingia ndani alimuona Flora ndiye mwenye mgahawa akisaidiana na kijana wa miaka 16 ambae ni picha ya Kichepe.

Kichepe alilia sana na kumuomba Flora msamaha. Flora alimwambia kwakua yeye ameokoka haweki vinyongo. Yaliyo pita yamepita lakini kwa sasa wamlee tu mtoto wao. Flora alihimiza mazoezi ya mama cheza mpaka Kichepe alianza kutembea lakini walibaki kuwa marafiki.
 
Back
Top Bottom