Kwani wanazokwapua wakiwa ofisini hazitoshi kuishi milele kwa raha mustarehe mpaka asumbuliwe na mafao ya uzeeni?
Kumbuka mafao ni kwaajili ya wenza wa viongozi wenu pia, WOTE WAKIWA HAWACHANGII sumni, wakipewa vinono kwa utumishi wa miaka michache.
Wanaochangia kwa miaka 36, wanapewa 33% tu ya haki yao na kuambiwa mwisho wa monthly pension ni miaka 12 ILHALI wasiochangia ambao wanalipwa mshahara kwa nafasi walizoomba wenyewe, wanalipwa mpaka KUFA.
Mtumishi kaongezewa tsh 23,000 kama nyongeza ya mshahara, IMETANGAZWA KITAIFA, MBUNGE kaongezewa MILIONI 5, hakuna aliyeambiwa! Ajabu, watumishi 500,000 hawana la kufanya...pathetic fools.
Hakuna serikali inaweza ku-replace watumishi 200,000 tu kwa pamoja; wapumbavu 400 Bungeni wanafaida gani ya nyongeza ya 5m monthly, kisha kulipwa 290m kama mafao kila baada ya miaka 5? Na ndio hao waliopitisha 33% kwa mtumishi wa miaka 36!
TUENDELEE TU kuhoji kwenye mitandao, WAO wanakwapua kihalisia!