Kichuya atwaa tuzo ya Mchezaji bora wa mwezi wa Tisa katika VPL.

sembo

JF-Expert Member
Joined
May 25, 2011
Posts
4,350
Reaction score
3,451
Mshambuliaji Shiza Kichuya wa Simba SC amechaguliwa kuwa Mchezaji Bora wa Ligi Kuu ya Vodacom kwa Septemba msimu wa 2016/2017.

Mchezaji aliisadia timu yake kwa mwezi huo kupata pointi zote 12 katika mechi nne ilizocheza, matokeo ambayo yameifanya Simba iendelee kuongoza Ligi hiyo inayoshirikisha timu 16. Pia alifunga mabao matatu katika mechi mbili kati ya nne ilizocheza timu yake.

Kwa kushinda tuzo hizo ya mwezi, Kichuya atazawadiwa kitita cha sh. 1,000,000 (milioni moja) kutoka kwa wadhamini wa Ligi hiyo, kampuni ya Vodacom Tanzania.

Kwa habari zaidi... [emoji116] [emoji116]

KICHUYA AMPIGA BAO KINGWANDE NA KUWA MWANASOKA BORA WA SEPTEMBA - SALEH JEMBE

Maoni Yangu: Nadhani hii tuzo alistahili mchezaji bora kabisa, Chirwa.. Hivi kina Jamal Malinzi hawajaona mchango wake Mkubwa katika timu yake + lile goli la kideoni?? Haiwezekani Bhana.. [emoji3][emoji3][emoji3]
 
Reactions: PNC
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…