Kichuya mchezaji bora wa mechi ya Mbao FC dhidi ya Simba

kirerenya

JF-Expert Member
Joined
Aug 27, 2013
Posts
1,696
Reaction score
2,253

Kiungo mahiri wa wekundu Msimbazi, Shiza Ramadhani Kichuya amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa mechi iliyopigwa jana dhidi ya Mbao FC mchezo uliyopigwa katika viunga vya CCM Kirumba uliopo Jijini Mwanza.

Hayo yamewekwa wazi na taarifa iliyotolewa na ukurasa maalum wa Simba SC usiku wa kuamkia leo baada ya kiungo huyo kuisaidia timu yake kwa kuipatia bao la kwanza kwenye mchezo dhidi ya Mbao FC, katika mechi ya ufunguzi wa mzunguko wa nne katika michuano ya Ligi Kuu Tanzania Bara inayoendelea kutimua vumbi.

"Kiungo mahiri Shiza Kichuya amechaguliwa na wapenzi wa Simba kuwa mchezaji bora wa mechi dhidi ya Mbao FC. Shiza kichuya amekuwa akifanya vizuri katika nafasi ya kiungo mchezeshaji pia kweye safu ya ushambuliaji na hivyo kumfanya kuwa kiungo muhimu kwenye kikosi cha Simba", imesema taarifa hiyo.

Shiza Kichuya anakuwa mcheza wa pili kuchaguliwa na timu yake kuwa mchezaji bora tokea ilipoanza michuano ya Ligi Kuu Tanzania Bara.

EATV
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…