Kunguru Mjanja
JF-Expert Member
- Aug 22, 2012
- 2,046
- 3,971
Mshambuliaji wa Simba na Taifa Stars, Shiza Kichuya amesema wakati wake ukifika atakwenda kucheza soka la kulipwa nje ya nchi kwani kila kitu hupangwa na Mungu.
Kichuya alisema bado anaendelea kupambana ili kuhakikisha anafanya vizuri na siku moja aweze kucheza soka la kulipwa nje ya nchi kama ilivyo kwa Mbwana Samatta na Simona Msuva.
"Hao wanaocheza sasa nje wakati wao umefika hata mimi naamini wakati wangu utafika tu kwani kila kitu ni Mungu anapanga. Muhimu ni kuongeza juhudi,” alisema Kichuya.
"Sijapata ofa yoyote kutoka nje zaidi ya kusikia tu natakiwa na timu za nje, lakini hakuna taarifa rasmi, hata hivyo sikati tamaa bado naendelea kupambana kuhakikisha naisaidia klabu yangu na timu ya Taifa na hayo mambo ya kucheza nje yatakuja tu,"alisisitiza Kichuya.
Kichuya amewahi kuhusishwa kutakiwa na timu moja ya Misri na Afrika Kusini ingawa uongozi wake ulikanusha madai hayo.
Mwananchi