benzemah
JF-Expert Member
- Nov 19, 2014
- 1,533
- 3,187
Utekelezaji wa Mtaala mpya kuanza Januari 2024
Mnamo tarehe 02 Novemba 2023, Mhe. Kasim Majaliwa Majaliwa(Mb.), Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, alitoa taarifa rasmi juu ya kuidhinishwa kwa Sera ya Elimu na Mafunzo 2014, Toleo la 2023 na Mitaala ya Elimu Ngazi ya Elimu ya Awali, Msingi, Sekondari na Elimu ya Ualimu.
Pamoja na mambo mengine alielekeza kuwa “.OR-TAMISEMI itakuwa na wajibu wa kuratibu na kusimamia Tawala za Mikoa zenye jukumu la kutekeleza Sera kwa kutoa elimu na Mafunzo katika ngazi ya Awali, Msingi na Sekondari...”
Ofisi ya Rais – TAMISEMI imepokea maelekezo ya kisera kutoka Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia juu ya utaratibu wa utekelezaji wa Mtaala mpya; ambapo baadhi ya Shule za Sekondari zimepangwa kutekeleza mkondo wa Amali za kihandisi na zinginezo.
Chanzo OR-TAMISEMI