Kidato cha pili mlioingia kidato cha tatu, chini ya wastan poleni

Kidato cha pili mlioingia kidato cha tatu, chini ya wastan poleni

fikirini

Senior Member
Joined
May 24, 2011
Posts
114
Reaction score
22
Kama kawaida ya serikali hii sikivu, baada ya kuchakachua matokeo ya kidato cha nne 2012 , sasa wamehamia kidato cha pili ...wameshusha alama hadi wastan wa alama 20, kama haitoshi wakasema basi wote waingie kidato cha tatu. wakati hili likifanyika wakuu wa shule wameamriwa kuwasimamia walimu wa masomo kuendesha masomo ya ziada kwa wale wanafunzi waliofeli na wale wenye wastan mdogo. Ndugu walimu, kweli hapa kuna uhalisia? haya masomo ya ziada ndiyo suluhisho,? je walimu mmeandaliwaje katika kutekeleza . wadogo zangu mliohurumiwa kuendelea kidato cha tatu, poleni, msipojisimamia wenyewe msitegemee miujiza.
 
Nafanya mchakato wa kufungua kec mahakaman dhid ya serikal kwa wale watoto waliofelisha mwaka jana na kulazimishwa kurudia kdato cha2
 
Futeni mitihani ya darasa la 4 & form II. Mitihani imezidi. Mnazidisha torture & terror kwa watoto.
 
Hapo hapo wanataka hao waliofaulu kwa wastani wa F form two wakifika form four wapate div 1-3.... Huu si usengerema??!!
 
Kama kawaida ya serikali hii sikivu, baada ya kuchakachua matokeo ya kidato cha nne 2012 , sasa wamehamia kidato cha pili ...wameshusha alama hadi wastan wa alama 20, kama haitoshi wakasema basi wote waingie kidato cha tatu. wakati hili likifanyika wakuu wa shule wameamriwa kuwasimamia walimu wa masomo kuendesha masomo ya ziada kwa wale wanafunzi waliofeli na wale wenye wastan mdogo. Ndugu walimu, kweli hapa kuna uhalisia? haya masomo ya ziada ndiyo suluhisho,? je walimu mmeandaliwaje katika kutekeleza . wadogo zangu mliohurumiwa kuendelea kidato cha tatu, poleni, msipojisimamia wenyewe msitegemee miujiza.

Kaka usiwatishe serikali iko makini kushughulikia suala la elimu inchini, kuna mpango wote wakaenda form 5 ili kupanua wigo wa elimu ya juu. Hata kama hawajui kusoma watajua mbele kwa mbele. Kunapromo nyingine inakuja inaitwa cheka time watapelekwa wote form 5 kisha tutamalizana nao na promo nyingine inaitwa happy hour ambapo wote watapelekwa vyuo vikuu hata kama hawajui kusoma watajua mbele kwa mbele. BRN ndio imeanza sasa na ari zaidi,kasi zaidi na nguvu zaidi.
 
duuuuh hv jaman kwa wale wa QT huwa wanafanya masomo mangapi kwa form two???na wanaingia form 3 kwa wastani upi,
 
Back
Top Bottom