Kidau na TFF wamesogeza kuni jirani ya moto, Simba wameona isiwe tabu, wamezichochea ziwake

marcoveratti

JF-Expert Member
Joined
Sep 21, 2017
Posts
1,019
Reaction score
1,824
Bifu zito linazidi kupambana moto kati ya Simba na Tff ya Kidau na karia.

Kuondolewa kwa wachezaji wa Simba kwenye kikosi cha timu ya taifa kinyume na sheria ndio sababu ya Bifu hilo, baada ya kidau kutangaza majina hayo ya wachezaji waliotemwa bado mgogoro unaendelea baada ya Kidau kuendelea kuwasema hovyo wachezaji waliotemwa.

Mvutano uliopo ni kuhusu kufuata utaratibu au kufuata sheria, viongozi wa Simba wanataka kufuata sheria na sio utaratibu aliojiwekea mtu, Amunike anataka aonekane ni mkubwa kuliko sheria? "aya ni maneno ya Wanasimba.

Sheria za soka zinasema,, mchezaji anamasaa 72 kutoka kwenye klabu yake na kwenda timu ya taifa, napia mchezaji anamasaa 24 kutoka timu ya taifa kwenda kwenye klabu yake,.

Pamoja na hayo yote, wanasimba nchini wamegoma kuisapot timu ya taifa na wataizomea popote pale itakapocheza mpaka Kidau na Amunike waanze kufuata sheria na sio utaratibu wanaojipangia na wake zao manyumbani mwao,.

Mashabiki wa Simba wameenda mbali zaidi kwa kumdai Golikipa wao Aishi Manula arudishwe na kama ataumia akiwa na timu hiyo basi wao awatahusika kumuuguza huku wakitolea mfano ilivyokuwa kwa Kapombe,. Ikumbukwe Kapombe aliumia ndani ya Taifa Stars lakini msala wa kumuuguza ulibaki kwa Simba wenyewe.

Kuanzia asubuhi ya leo baadhi ya mashabiki wameanza kuweka profile zao picha ya timu ya Uganda wakimaanisha watakuwa upande wa Uganda siku ya Tarehe 8 mwezi unaokuja.

tapatalk_1535554743702-01.jpeg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hata kama viongozi walikosea ila suala wa simba kuisapoti uganda ni upumbavu, bora wapige kimya.
Haya mambo ya fitina za kiushabiki watuachie sisi mashabiki, wao bado wanaishi kwenye ulimwengu wa soka, soka ndio ajira yao, makosa ya leo yasiwaharibie kile kile walichokijenga kwa miaka mingi
 
Mashabiki mbùmbumbu Tanzania

Walishawahi kung'oa viti uwanjani
 
Bifu zito linazidi kupambana moto kati ya Simba na Tff ya Kidau na karia.

Kuondolewa kwa wachezaji wa Simba kwenye kikosi cha timu ya taifa kinyume na sheria ndio sababu ya Bifu hilo, baada ya kidau kutangaza majina hayo ya wachezaji waliotemwa bado mgogoro unaendelea baada ya Kidau kuendelea kuwasema hovyo wachezaji waliotemwa.

Mvutano uliopo ni kuhusu kufuata utaratibu au kufuata sheria, viongozi wa Simba wanataka kufuata sheria na sio utaratibu aliojiwekea mtu, Amunike anataka aonekane ni mkubwa kuliko sheria? "aya ni maneno ya Wanasimba.

Sheria za soka zinasema,, mchezaji anamasaa 72 kutoka kwenye klabu yake na kwenda timu ya taifa, napia mchezaji anamasaa 24 kutoka timu ya taifa kwenda kwenye klabu yake,.

Pamoja na hayo yote, wanasimba nchini wamegoma kuisapot timu ya taifa na wataizomea popote pale itakapocheza mpaka Kidau na Amunike waanze kufuata sheria na sio utaratibu wanaojipangia na wake zao manyumbani mwao,.

Mashabiki wa Simba wameenda mbali zaidi kwa kumdai Golikipa wao Aishi Manula arudishwe na kama ataumia akiwa na timu hiyo basi wao awatahusika kumuuguza huku wakitolea mfano ilivyokuwa kwa Kapombe,. Ikumbukwe Kapombe aliumia ndani ya Taifa Stars lakini msala wa kumuuguza ulibaki kwa Simba wenyewe.

Kuanzia asubuhi ya leo baadhi ya mashabiki wameanza kuweka profile zao picha ya timu ya Uganda wakimaanisha watakuwa upande wa Uganda siku ya Tarehe 8 mwezi unaokuja.

[Source www.instagram.com/mwanaspotiapp]View attachment 851919

Sent using Jamii Forums mobile app
Usituunganishe mashabik wa simba na ushamba wenu, wachezaj wanatakiwa kubadilika sasa. Hao mabishoo walijichelewesha tu mbona aish aliweza kureport mapema. Pamoja na yote kocha ameita wachezaj wazur, Nina imani na Kelvin kongwe sabato "kiduku"

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tz hata afcon kufuzu taabu lkn kocha anahitaji watu kambini mapema kwa faida ya taifa wanakuambia sheria za fifa siku 3..ahaa wap..lazima tujiongezee lazima tutoke nje ya sheria tutoke jasho tuone mafanikio hata kidogo kwenye soka letu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Busara itumike ili kuweka mshikamamo wa kitaifa...hao tff na simba wakiendelea kuvimbiana madhara yataikumba nchi na wala si wao
 
Wachezaji wetu wa Kibongo wasipokuwa na nidhamu wataishia hapa hapa Simba na Yanga........Kipa wa Simba aliwahi kambini kwanini hao wengine wachelewe?

Tatizo wachezaji wetu wakishacheza Simba na Yanga, wakawa na wafuasi 1000 kwenye mitandao ya kijamii wanaona wameshamaliza kazi, wanaanza kiburi na dharau.

Alichofanya kocha wa Taifa stars ni sahihi ili kurudisha nidhamu kwa wachezaji na sisi mashabiki tuache Usimba na Uyanga kwenye timu ya taifa.
 
Back
Top Bottom