SoC02 Kidawa

Stories of Change - 2022 Competition

Actuality

Member
Joined
Jul 30, 2022
Posts
7
Reaction score
10
“KIDAWA”
UTANGULIZI

Jioni kama saa 12 hivi na dakika zake, binti mrembo katika kijiji cha Mwembeni, akitoka kuchota maji kisimani ghafla wanatokea vijana wawili wenye nguvu wanamsimamisha na kuanza mazungumzo nae, kabla mazungumzo hayajaisha binti yule anatupa ndoo chini na kuanza kukimbia huku vijana wale wakimbimbiza kwa nyuma. Hawakwenda mwendo mrefu sana na tayari vijana wale walisha mkamata na kutaka kumbeba juu juu huku binti yule akionesha hataki kwa kukataa kwa nguvu zake zote.

Kijana1: Tulia wewe tukwambie mara ngapi bosi anakuhitaji

Binti: Nimesema sitaki, mwambieni sitakii

Kijana2: Oya tuachane nae tumwambie tumemkosa tu

Kijana1: Weeeeee humjui yule mzee, akiangalia kwenye kimbora yake hatulali leo. Bora tumpeleke tu kwa usalama wetu

Binti: mniachee, jamaaani eeehhh nabakwaaaa hukuuu mnisaidieee(akipiga kelele kuomba msaada)

Hakuna aliyeonekana kwenda kumsaidia walimbeba hadi kwa mzee Mkwaju, mwenyekiti wa kijiji cha Mwembeni. Kwanini wamempeleka kwa mwenyekiti kwa nguvu?

MWEMBENI NA MKWAJU
Kijiji cha Mwembeni ni kijiji kilichopo pembezoni kabisa ya Mkoa karibu na nchi jirani. Mwenyekiti wa kijiji hicho anaitwa mzee Mkwaju, mzee mkatili sana, anasifika kwa ukatili na utawala wa kutumia mabavu.

Hakuna wa kumpinga, akitokea wa kumpinga atakutwa kafariki katikati ya kijiji sokoni. Ana mwaka 10 sasa yeye ndiyo mwenyekiti pekee kuwahi tokea kijijini hapo

Alikuwa na tabia ya kubaka wasichana kila mwisho wa wiki na hupelekewa nyumbani kwake kwa kukamata kwa nguvu mabinti wadogo kabisa wa umri kuanzia miaka 10 na Kuendelea na vijana wake wanaomfanyia kazi ya kukamata watu mbalimbali.

Huwafanyia ubakaji wasichana wengi sana hapo kijijini isipokuwa wachache tu. Wengine hujipeleka wenyewe kwa kutaka maisha rahisi na ufahari hapo kijijini nao waliambulia kubakwa na kuachwa na ujauzito kisha kufukuzwa kwa mzee Mkwaju. Hivyo kuna watoto wengi kijijini wa mzee Mkwaju na amewakataa.

HARAKATI ZA KIDAWA

Mtu pekee anayeendesha harakati za kumpinga mzee Mkwaju ni binti mdogo kabisa wa miaka 19, mrembo na mwenye maarifa anayeitwa KIDAWA. Kidawa naye ni muhanga wa kubakwa na mzee Mkwaju. Siku alipotoka kwenda kijiji kingine kumtembelea dada yake, alipata homa kali sana na alipopelekwa hospitali baada ya kupimwa na matibabu akagundulika kuwa ana virusi vya ukimwi na kupewa elimu kuhusu HIV.

Kidawa alilia sana kwa uchungu kusikia kuhusu HIV na ilifikia hata kujuta kuzaliwa kijiji cha Mwembeni. Lakini kutokana na elimu aliyopata akaamua kurudi kijijini kwao kuja kuwakomboa mabinti wengine ambao wameathirika kama yeye na kuwasaidia wale wengine ambao bado hawajapata ugonjwa huo. Kabla hajarudi kijijini alitoa taarifa za kijijini kwao kwa viongozi wa kjjiji alichofikia kwa dada yake na wao wakampa ahadi watatoa taarifa katika serikali ya wilaya. Kidawa akaamua kurudi kijijini kwao.

KIDAWA NA ELIMU YA UKIMWI
Alipofika kijijini kwao alianza kutoa elimu kwa mabinti mbalimbali kuhusu ugonjwa wa HIV. Baada ya mwezi kina mama nao wakajiunga kwenda kupata elimu hiyo kwa kidawa. Elimu hiyo kidawa aliitoa kwa siri sana hasa muda wa usiku alipokuwa akiwatembelea mabinti wenzake. Vijana wa kiume nao wakaanza kuhamasika baada ya kupewa taarifa na mama zao. Ndani ya mwezi mmoja na nusu tayari kidawa alishatoa elimu karibia kwa robo ya vijana wote kijijini kwao. Siku ya siku mzee Mkwaju akajua baada ya kupewa taarifa na binti mmoja aliyeenda kuchunguza harakati za Kidawa.

HASIRA ZA MKWAJU

Mzee Mkwaju alikasirika sana, akaanda adhabu kali kwa ajili ya kidawa. Akaandaa vijana wake wenye nguvu ili wamsubirie kidawa akitoka tu usiku kwenda kutoa elimu wamkamate na kumpeleka kwake kwa ajili ya adhabu.

Basi ilipofika usiku, kidawa anatoka tu kwao kupiga hatua kadhaa akawa kazungukwa na vijana wale wenye nguvu. Kidawa alistuka sana akajaribu kuomba msaada na kupiga kelele hakuna aliejaribu kutoka kumsaidia kidawa, kidawa alitia huruma sana akakaa chini kwa kukosa matumaini na kuanza kulia akijua sasa mwisho wa maisha yake umefika, hata wazazi wake hawakuthubu kutoka. Vijana wale wote walikuwa wameshika magongo na fimbo, kidawa kwa kuona hivo akajua basi mwisho wake umefika.

Wakati amejiinamia pale chini akimuomba mungu abadilishe maamuzi na akisali sala zake za mwisho, akijua kabisa kesho asubuhi atakutwa sokoni kafariki. Ghafla akasikia sauti ambayo hakuitarajia iliyofufua matumaini yake.

Kijana2: kidawa unalia nini dada? Upo mikono salama kwa sasa tuambie tufanye nini uwe salama umetusaidia sana kwa kutupa elimu lakini wenzetu wengi wanakufa na ugonjwa na hata hatujui dawa yake

Kidawa: Eeehhhh?

Kijana2: sema tufanyaje kabla wenzetu hawafika ambao ni waaminifu kwa mzee

Kidawa: Tuondoke twende kijiji cha pili nilishatoa taarifa ya kijiji.

Kijana2: Tuongoze dada tupo hapa kwa ajili yako

Basi wakaondoka usiku ule huku kidawa akiwa bado haamini macho yake na akihisi kama anaota hivi vijana wale kama wanne hivi walimsindikiza kijjji cha pili kidawa

Huku nyuma mzee Mkwaju alimtafuta kidawa na wale vijana akiwa na vijana wengine hakuwapata akaamua kukamata wazazi wa kidawa na akaanza kutoa adhabu ili wataje kidawa alipo, lakini hawakuweza kutaja.

UKOMBOZI MWEMBENI
Wakati Kidawa na wale vijana wako safarini usiku ule wamefika katikati ya safari wakasikia sauti ya gari wakajificha kidogo, baada ya kidawa kuliona lilie gari akalikumbuka na kujitokeza mafichoni kulisimamisha. Lilikuwa ni gari la polisi likiwa na askari, mwenyekiti wa kijiji anachoishi dada yake na dada yake wakija kijijini kwao kufuatilia taarifa alizotoa kidawa. Kidawa alifurahi sana akawatambulisha wale vijana na kuwaambia polisi kuwa hapo yupo anakimbia hasira za mzee Mkwaju. Basi wote wakapanda kwenye lile gari na kuanza kurudi kijijini Mwembeni.

Walifika kama saa tisa usiku, watu waliokuwa nje wakishuhudia adhabu pamoja na mzee Mkwaju walishaangaa na hapo hapo polisi walishuka na silaha zao na kuwakamata mzee Mkwaju na vijana wake na kuwasaidia mama na baba yake Kidawa kuachwa huru.

Mzee Mkwaju alitaka kugoma na kuleta tafrani kidogo lakini polisi walitumia weledi wao kuwakamata ipasavyo na kuacha kijiji huru.

Kumbe wanakijiji walikuwa wanasikia walitoka nje kushangilia, walimbeba Kidawa juu huku wakicheza na kuimba kwa kufurahi.

KIDAWA BINGWA DHIDI YA UKIMWI NA UTAWALA WA MABAVU

Baada ya siku mbili serikali ilituma wataalamu wa afya kwenda kutoa elimu na vipimo vya afya hasa HIV pamoja na kupeleka dawa mbalimbali kwa wagonjwa, ambapo waathirika wakubwa walikuwa vijana wakike. Wanakijiji wa Mwembeni walipelekewa misaada na Kidawa akapewa kazi katika shirika la ukimwi na kuanza kutoa elimu katika vijiji kuhusu gonjwa la ukimwi.
 
Upvote 5
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…